• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RAIS MAGUFULI AKABIDHIWA TAARIFA YA MATOKEO YA UHAKIKI WA VYETI KWA WATUMISHI WA UMMA APRILI 28, 2017

Imetumwa : April 28th, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Leo Aprili 28, 2017 amepokea taarifa ya uhakiki wa vyeti kwa Watumishi wa Umma katika ukumbi wa Chimwaga Dodoma na kuagiza Wizara ya Fedha kuwaondoa katika orodha ya Watumishi wa Umma na kusimamisha mishahara ya Watumishi 9,932 waliobainika kutumia vyeti vya kugushi.

Idadi ya Watumishi hao imebainika baada baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa Angela Kairuki kukabidhi taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti kwa Watumishi wa Umma zaidi ya laki nne kwa Rais Magufuli, zoezi ambalo liliendeshwa na Serikali kuanzia mwezi Oktoba mwaka 2016.

Rais Magufuli pia amewataka Watumishi 9,932 waliobainika kutumia vyeti vya kughushi kujiondoa wenyewe katika Utumishi wa Umma kabla ya tarehe 15 Mei, 2017 na baada ya muda huo hatua za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

“Kwa hiyo Waziri Mkuu upo hapa na Waheshimiwa Mawaziri wote mnaohusika, hawa watu 9,932 mshahara wao wa mwezi huu ukatwe na waondoke mara moja kwenye Utumishi wa Umma kuanzia leo, watakaobaki mpaka tukiingia mwezi wa tano tuwapeleke kwa mujibu wa sheria ili kusudi wakafungwe hiyo miaka saba” amesema Rais Magufuli.

Pia Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kutangaza nafasi hizo 9,932 upya ili wenye sifa stahiki waweze kuomba.

Aidha, Rais Magufuli ameiagiza Tume inayofanya uhakiki wa vyeti kwa Watumishi wa Umma kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu kuendelea na uchunguzi wa Watumishi wa Umma 1,538 waliobainika kutumia vyeti vyenye utata hadi Mei 15, 2017.

“Hawa wenye vyeti vya utata kwa maana kuwa vyeti vyao vinatumiwa na watu zaidi ya mmoja, Wizara ya Utumishi muhakikishe kufika tarehe 15 muwe mmeshajua ni nani mwenye cheti chake, na mshahara wa mwezi huu wasipewe kwanza mpaka atakayepatikana mwenye cheti halali” amesema Rais Magufuli.

Pia ameagiza uchunguzi ufanyike kwa Watumishi 11,596 wenye vyeti vya utaalamu bila kuwasilisha vyeti vya kidato cha sita kwa kuwa sio fani zote zinazohitaji kuwa na vyeti vya kidato cha sita ili kusomea utaalamu husika na kuagiza kulipwa mishahara yao kama kawaida.

Katika hatua nyingine , Rais Magufuli amezindua Maadhimisho ya miaka kumi (10) tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dodoma.

Rais Magufuli amewaeleza Wanajumuiya ya Chuo Kikuu cha Dodoma mipango mbalimbali inayofanywa na Serikali katika kuboresha maisha ya Watanzania na kukuza Uchumi ikiwa ni pamoja na kuimarisha miundombinu ya Usafiri kwa kununua ndege mpya sita (6) na Ujenzi wa Reli ya Kisasa (Standard Gauge).

Mheshimiwa Rais amesema hatua ya Serikali kuimarisha huduma za jamii inatokana na mafanikio ya Serikali kudhibiti upotevu wa mapato na hivyo kuwataka wananchi kuunga Mkono jitihada za Serikali ili kukamilisha malengo ya Tanzania ya Viwanda.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2020 January 15, 2021
  • MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2020 January 15, 2021
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021 SHULE ZA BWENI (WASICHANA NA WANAUME) . December 20, 2020
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA YA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2020 January 15, 2021
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KATIBU TAWALA SINGIDA AKABIDHI OFISI KWA KATIBU TAWALA DODOMA

    March 23, 2023
  • MACHINGA DODOMA WAMPONGEZA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

    March 23, 2023
  • KIWANDA CHA AINA YAKE KUJENGWA KONGWA

    March 17, 2023
  • WAFANYAKAZI WAASWA MSHIKAMANO MAHALA PA KAZI

    March 15, 2023
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Mkoa akiongoza siku ya maombi jijini Dodoma
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.