• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC SENYAMULE AWAHIMIZA WANADODOMA KUJITOKEZA KUPIGA KURA

Imetumwa : November 27th, 2024

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS

Wito umetolewa kwa Wakaazi wa Mkoa wa Dodoma kufika katika vituo walivyojiandikishia kwa ajili ya kutimiza haki ya kidemokrasia kwa kushiriki kupiga kura kuchagua Viongozi wa Serikali za Mitaa yao pamoja na kulinda amani.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule aliposhiriki zoezi hilo katika kituo chake alichojiandikishia Shule ya Msingi Dodoma Mlimani, Mtaa wa Salmini, Kata ya Tambukareli Jijini Dodoma mapema leo Novemba 27, 2024.

“Siku ya leo ni ya muhimu sana Dodoma kuwa salama. Tukumbuke kauli yetu ‘Uchaguzi salama kwa maendeleo ya Taifa letu’. Nitoe wito kuwa asikose mtu kwenda kupiga kura kwenye kituo alichojiandikishia na kila mmoja ahakikishe analinda usalama” Amesisitiza Mhe. Senyamule

Kadhalika, amewashukuru wana Dodoma wote kwa kuendelea kutunza amani na utulivu wakati wote tangu kuanza kwa mchakato wa Uchaguzi, wakati wa kampeni hadi leo hii  unapokwenda kutamatika.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya,  amepiga kura katika kituo alichojiandikishia Mtaa wa Mathias, Kata ya Miyuji, Jijini Dodoma na kutoa hamasa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwani vituo vipo karibu na makaazi ili kutimiza haki ya kuchagua viongozi wanaowataka.

Miongoni mwa viongozi wastaafu wa Mkoa wa Dodoma aliyepata nafasi ya kushiriki zoezi hilo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ni Bw. Peter Mavunde (Meya mstaafu wa Jiji la Dodoma) ambapo ametoa hamasa kwa wanachi kujitokeza mapema, kwa wingi   kwenye vituo vya kupigia kura ili kutimiza haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi watakaowafaa.

“Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi”


#kurayakosautiyako              

#ujanjanikupigakura              

#dodomatukotayarikupigakura

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • DHAMIRA YA MHE.RAIS , WATANZANIA KUPATA HUDUMA YATIMIA KWA MKOA WA DODOMA

    May 22, 2025
  • WAKANDARASI WASIOKAMILISHA MIRADI KUDAIWA FIDIA

    May 21, 2025
  • KUBORESHA LISHE NGAZI YA KAYA; KAMATI YA LISHE MKOA WA DODOMA YADHAMIRIA KUWA MFANO

    May 18, 2025
  • TANZANIA NCHI YA KWANZA AFRIKA MASHARIKI KUZALISHA TANI 34,000 ZA ASALI

    May 20, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.