• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

VIJANA MKOANI DODOMA KUPATA UFADHILI KWENYE MIRADI YA UZALISHAJI KIBIASHARA

Imetumwa : June 30th, 2018

VIJANA MKOANI DODOMA KUPATA UFADHILI KWENYE MIRADI YA UZALISHAJI KIBIASHARA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge mwishoni mwa wiki amekutana na Ujumbe wa Viongozi wa Kampuni ya Uranium One ya Nchini Urusi inayoendesha shughuli za madini hapa nchini na kufanya mazungumzo juu ya masuala ya maendeleo na uwekezaji ambapo Dkt. Mahenge alitumia fursa hiyo kuushawishi uongozi wa Kampuni hiyo kupitia kitengo chake cha Uhusiano na huduma kwa jamii kufadhili mradi wa Kambi za Vijana za Uzalishaji kibiashara aliouanzisha kwa lengo la kuzalisha ajira kwa vijana na kuwawezesha kujipatia kipato ili kujitegemea.

Dkt. Mahenge alimjulisha Rais wa Kampuni ya Uranium One Ndg. Vasiliy Kostantinov aliyekuwa ameambatana na Afisa wa Ubalozi wa Urusi hapa nchini anaeshughulikia masuala ya uchumi Ndg. Kivill Bellikov kuwa Uongozi wa mkoa wa Dodoma umeanzisha mradi wa Kambi za Vijana za Uzalishaji Kibiashara kwa kutumia fursa zinzaopatikana kwenye maeneo mbalimbali ya Mkoa ambapo jukumu kubwa la Uongozi wa Mkoa ni kuwawezesha vijana mitaji na mahitaji muhimu ikiwa ni pamoja na mafunzo ya utaalamu na kuwasimamia katika miradi hiyo ya uzalishaji ili waweze kuzalisha kwa tija na kujipatia kipato.

Aliongeza kuwa miradi ya mwanzo Mkoa ulioanza nayo ni pamoja na Kambi ya Kilimo cha Umwagiliaji mbogamboga na matunda eneo la Chikopelo Bahi, ambapo fursa ya kipekee kwenye eneo hilo ni pamoja na Ardhi ya kutosha yenye rutuba nzuri na uwepo wa Bwawa la Chikopelo ambalo halikauki maji yake kipindi chote cha mwaka hivyo vijana wakiwezeshwa wanaweza kufanya kilimo cha Umwagiliaji kwa kipindi chote cha mwaka na wakalisha jiji la Dodoma kwa mahitaji ya mboga na matunda ukizingatia idadi kubwa ya wafanyakazi na viongozi wa Serikali wamehamia Mkoani Dodoma.

“Kwa kushirikiana na uongozi wa Wialaya ya Bahi na Mbunge wa Bahi Mhe. Omari Baduwel tumewatengea vijana pale Chikopelo jumla ya shilingi milioni 15 kwa ajili ya kupata mahitaji muhimu na mashine za kuvutia maji kwa ajili ya kuanza mradi wa umwagiliaji mbogamboga” alijulisha Dkt. Mahenge.

Vilevile Dkt. Mahenge aliueleza ujumbe huo kuwa mradi wa pili wa kambi ya Vijana ya Uzalishaji kibiashara ni mradi wa uzalishaji Matofali na Vifaa vingine vya Ujenzi utakaokuwa na kambi hapa Jijini Dodoma ambapo tayari vijana wa kujiunga na kambi hiyo wameshafanyiwa usaili na eneo kwa ajili ya kambi hiyo ya uzalishaji tofali limeshapatikana. Aliongeza kuwa Uongozi wa Mkoa ulipata msaada wa mashine kumi (10) za kufyatulia tofali kutoka kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na hivyo kuamua kuzitumia mashine hizo kwa kuanzisha mradi wa vijana wa uzalishaji tofali ukizingatia kwa sasa mahitaji ya matofali na vifaa vingine vya ujenzi ni makubwa kwa kuwa taasisi mbalimbali zipo kwenye harakati za kutengeneza majengo yao ya Ofisi, makazi na huduma mbalimbali hapa Mkoani Dodoma halikadhalika ujenzi wa miundombinu mbalimbali unaoendelezwa kwa sasa hapa Makao Makuu ya Nchi.

Rais wa Kampuni ya Uranium One Ndg. Vasiliy Kostantinov amepongeza jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge za kuanzisha miradi inayozalisha ajira kwa vijana na ameahidi kuwa kampuni yake kwa pamoja na Ubalozi wa Urusi hapa nchini watashirikiana na Uongozi wa Mkoa wa Dodoma kwenye eneo hilo la miradi ya vijana ya Uzalishaji kibiashara na umeahidi kufadhili miradi hiyo ili kuzalisha fursa nyingi zaidi kwa vijana.

Aidha, ameomba Uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Dodoma kuwasilisha Andiko la miradi hiyo ya vijana kwa ubalozi wa Urusi kwa ajili ya kufahamu mahitaji muhimu na gharama zake ili kuanza uratibu wa upatikanaji wake.

Katika hatua nyingine, Katika mzaungumzo hayo Mkuu wa Mkoa Dkt. Mahenge alielezea kuwa uongozi wa Mkoa kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali unatarajia kufanya Kongamano Kubwa la Uwekezaji ambapo Kongamano hilo linatarajiwa kuwa kubwa na la aina yake na kuwa litakaribisha wadau hapa nchini Tanzania na kutoka nje ya nchi.

Aliongeza Kongamano hilo litatumika kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Mkoani Dodoma Makao Makuu ya Nchi na kukaribisha Wawekezaji wenye nia kuja kuwekeza Dodoma. Kufuatia Mpango huo, Rais wa Kampuni ya Uranium One Ndg. Vasiliy Kostantinov amesema kwa pamoja na Ubalozi wa Urusi hapa Nchini watashirikiana na Uongozi wa Mkoa wa Dodoma kufadhili na kushiriki maandalizi ya kongamano hilo na kuwa wataleta wawekezaji kutoka nchini Urusi kuja kushiriki kwenye Kongamano hilo hapa Mkoani Dodoma.

Katika kumalizia mazungumzo yao, ujumbe huo kutoka ubalozi wa Russia hususani upande wa Kampuni ya Uranium One umekubaliana na Uongozi wa Mkoa wa Dodoma kuanzisha mashindano ya Riadha ya Mkoa wa Dodoma kama moja ya njia ya kukuza mchezo huo na pia kutumia tamasha hilo la riadha kuutangaza Mkoa wa Dodoma na fursa zake za utalii kama vile mapori ya Akiba ya Swagaswaga na Mkungunero kama moja ya maeneo ya utalii yatakayotumiwa na Wafanyakazi na wadau mbalimbali waliohamia hapa Mkoani Dodoma Makao Makuu kama sehemu ya mapumziko.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2020 January 15, 2021
  • MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2020 January 15, 2021
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021 SHULE ZA BWENI (WASICHANA NA WANAUME) . December 20, 2020
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA YA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2020 January 15, 2021
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KATIBU TAWALA SINGIDA AKABIDHI OFISI KWA KATIBU TAWALA DODOMA

    March 23, 2023
  • MACHINGA DODOMA WAMPONGEZA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

    March 23, 2023
  • KIWANDA CHA AINA YAKE KUJENGWA KONGWA

    March 17, 2023
  • WAFANYAKAZI WAASWA MSHIKAMANO MAHALA PA KAZI

    March 15, 2023
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Mkoa akiongoza siku ya maombi jijini Dodoma
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.