• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Akagua Maendeleo ya Ujenzi na Maendeleo ya Wanafunzi wa Kidato Cha Tano Katika Shule Za Sekondari KIbaigwa na Bunge

Imetumwa : June 30th, 2022

Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Bw. Gift Kyando, leo ametembelea shule ya Sekondari ya Wasichana Kibaigwa iliyopo katika Wilaya ya Kongwa  na Shule ya sekondari ya Wasichana Bunge iliyopo eneo la Kikombo, Wilaya ya Chamwino  Mkoa wa Dodoma. Bw. Kyando amefanya ziara hiyo yenye lengo la kuangalia maendeleo ya ujenzi na maendeleo ya wanafunzi kidato cha 5 walipokelewa shuleni hapo.

Shule ya Wasichana Kibaigwa, imejengwa kwa fedha za Serikali, ambapo Serikali ilitoa kiasi cha Tsh.1 bln, ambazo zimetumika kujenga Madarasa 13, Mabweni 4, Bwalo la chakula, jengo la utawala, nyumba za walimu pamoja na Maabara 2 kwa ajili ya masomo ya Sayansi.

Akizungumza Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Bi. Jema Kihwelu amemshukuru,Afisa Elimu Mkoa kwa Kutenga wakati na kutembelea shule hiyo ili  kuangalia maendeleo ya ujenzi wa shule pamoja na wanafunzi. Mwalimu Kihwelu ameahidi kushirikiana na walimu wenzake kufanya kazi kwa bidii  ili kuhakikisha shule yake hiyo inafanya vizuri katika matokeo yake ya Kidato cha Sita.

“Mimi ni Mama yenu, naahidi kuwalea, nitawapenda, kuwalinda na kuwasimamia katika masomo yenu na kuhakikisha munafanya vizuri katika mitihani yenu". Amesisitiza Mwl.Kihwelu.

Nae Afisa elimu Mkoa, Bw. Kyando  amewasaa wanafunzi  hao  kusoma kwa bidii.Nikiwa Afisa Elimu Mkoa Jukumu langu kubwa  ni kuhakikisha wanafunzi wote wa Mkoa wa Dodoma wanapata fursa ya kusoma shule na katika mazingira rafiki.

"Sisi wazazi wenu tumewaleta hapa musome na si vinginevyo, hivyo mi muhimu musome kwa bidii ili muje  kufaulu vizuri, na hatimae kutupatia sifa sisi wazazi wenu.Hivyo hakikisheni kila munapoamka,  mnapokula, mnapocheza na mpolala, akili yenu iwe inafikiria masomo tu. Ni vyema kila mmoja wenu ajiulize nitapelekea zawadi gani kwa wazazi wangu endapo nitafeli? Serikali inajitahidi sana kuwaletea huduma zote zinazohitajika na kuwajengea mazingira rafiki kwa masomo, ili kazi ya kusoma tu ibaki kwenu, hivyo hakikisheni kitabu kinakua kipaumbele kila mnapoamka mpaka mnapolala". Amesisitiza Bw. Kyando.

Shule ya Sekondari ya Wasichana Kibaigwa ni miongoni mwa shule 30 za kidato cha Tano na Sita zilizopo katika Mkoa wa Dodoma na inatarajiwa kupokea wanafunzi 204, mpaka Sasa jumla ya wanafunzi waliowasili shuleni hapo ni 147 tu. Shule hiyo inafundisha michepuo ya CBG, HGE, EGM na HGK huku ikiwa na walimu 13 ambapo kwa Sasa wapo waalimu 8 wakati walimu wengine watano watawasili  siku chache zijazo.

Aidha baada ya ziara hiyo, Afisa Elimu amtembelea Shule ya sekondari ya Wasichana Bunge iliyopo eneo la Kikombo, Wilaya ya Chamwino kujionea maendeleo yake na pia kuongea na wanafunzi ambapo pia amewaasa wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza malengo yao nakurudisha zawadi nono Kwa wazazi na walezi wao.

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’ YAIVA

    May 08, 2025
  • DODOMA YADHAMIRIA KUJIKITA KWENYE KILIMO CHA MATUFAHA (APPLES) KUINUA UCHUMI

    May 08, 2025
  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.