• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

BILIONI 16 ZIMEBORESHA MAZINGIRA YA KUJIFUNZIA NA KUINUA UFAULU MKOA WA DODOMA

Imetumwa : March 20th, 2025

Na. Hellen M. Minja,

       Habari - DODOMA RS


Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, imefanya jitihada kubwa kwa kuboresha miundombinu ya kujifunzia katika Mkoa wa Dodoma ambapo takribani shilingi Bilioni 116. 84 zimetumika katika Ujenzi wa shule mpya, madarasa, mabweni, maabara na miundombinu mingine kadha wa kadha.


Hayo yamebainishwa wakati wa hotuba ya Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Doto Biteko ambaye alikua mgeni rasmi kwenye Mkutano wa Wadau wa Elimu 2025 Mkoa wa Dodoma ambayo ilisomwa na Mwakilishi wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo Machi 20, 2025.


"Serikali imeendelea na Ujenzi wa miundombinu ya elimu ikiwemo shule mpya, madarasa, mabweni, maabara kupitia miradi mbalimbali ambapo imetumia takribani shilingi Bilioni 116. Aidha shilingi Bilioni 56 zimetolewa kama ruzuku kwa ajili ya elimu bure kuanzia awali hadi kidato cha sita. Serikali pia imetoa vyombo vya usafiri kwa Maafisa elimu Kata zikiwemo pilipili na magari 394 kwa ajili ya usimamizi wa miradi ya elimu" Mhe. Dkt. Biteko


Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Wilson Charles Mahela amesema katika uongozi wa Mhe. Rais Samia, wameshuhudia maboresho makubwa kwenye Sera na Mitaala ya elimu ambayo itasaidia wanafunzi pindi watakapomaliza masomo yao waweze kujiajiri kupitia mafunzo ya Amali yaliyoanza katika mwaka mpya wa masomo 2025.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema kuwa haya yanayotokea ndio lengo la Mhe. Rais Samia ndio maana Mkoa unampongeza leo kwani amechangia ongezeko la ufaulu Dodoma pia amewataka wanadodoma kutumia fursa za kiuchumi alizoziweka Mhe. Rais Mkoani hapa katika kuinua uchumi wao.


Kadhalika, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya amesema kazi aliyoifanya Mhe. Rais kuleta maendeleo katika sekta ya elimu Mkoa wa Dodoma ni kubwa na lengo lake ni kuongeza ufaulu katika ngazi zote kufikia 100% hivyo, katika miaka hii minne ya Mhe. Rais Dodoma imejipambanua kwa kuongeza ufaulu.


Akitoa tathmini ya ongezeko la ufaulu kwa Mkoa wa Dodoma kwa mwaka 2023 na 2024 kwenye Mitihani ya Upimaji na ile ya Taifa, Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Mwl. Vicent Kayombo amesema kwenye matokeo ya Upimaji darasa la Nne, ufaulu ulikua 92.50% (2023), umefikia 94.64% (2025), Darasa la Saba ufaulu 87.05% (2023) umefikia 87.89% (2025), kidato cha pili 84.85% (2023), umefikia 86.12% (2025) na kidato cha nne 87.63% (2023), umefikia 92.81% (2025).


Mkutano huo umefikia maazimio kadhaa ikiwemo kuhakikisha chakula cha mchana kinapatikana shuleni ili kudhibiti utoro, kuboresha ujifunzaji kwa kumaliza mada mapema na kufanya majaribio mengi, kila baada ya Mitihani, walimu wafanye tathmini ya namna ya kupandisha ufaulu na kuongeza miundombinu hususan hosteli ili kupunguza umbali wa kutembea kwa wanafunzi.


Mkoa wa Dodoma huandaa Mkutano wa Wadau wa Elimu kila mwaka wenye lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa shughuli za elimu na tathmini ya matokeo ya Upimaji na Mitihani ya Taifa. Katika Mkutano huo pia, tuzo mbalimbali hutolewa, vyeti vya pongezi na fedha taslimu ili kuamsha ari ya utendaji kazi kwa Walimu, wanafunzi na Watendaji wa Elimu kwa ujumla.




#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • KAMPUNI YA "CAVO'' YA CHINA YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

    May 05, 2025
  • TAWLA - SAUTI YA WANAWAKE NA WATOTO WALIOKOSA ULINZI WA KISHERIA KATIKA JAMII

    May 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.