• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

BILIONI 17 KUJENGA MNARA WA MASHUJAA NA UKUMBI

Imetumwa : April 20th, 2023


Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewapongeza wana Dodoma kwa miaka 59 ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar ikiwa ni wiki ya maadhimisho sherehe hiyo na kuwataka vijana kuchangamkia fursa zinazoendelea kujitokeza jijini Dodoma.

Senyamule ameyasema hayo leo alipotembea mradi wa ujenzi wa uwanja na mnara wa mashujaa katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba.

‘’Leo nina furaha kubwa kwa kuwa maelekezo ya Mhe Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa hapa jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2022 wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya mashujaa yanaendea kutekelezwa na hii ni heshma kubwa kwetu wana Dodoma kwakuwa Mradi huu kuanza kutekelezwa kwa vitendo. Kupitia mradi huu, tunakwenda kuweka alama nyingine muhimu itakayopendezesha Mkoa wetu ambao ndio Makao Makuu ya Nchi yetu, pia wanadodoma watanufaika kiuchumi na kijamii” Senyamule amefafanua

Aidha Mhe. Senyamule amewataka wakandarasi kuhakikisha wanatekeleza ujenzi wa mradi kwa hadhi kubwa na sifa nzuri kwa kuzingatia ubora na imara kwa miundombinu na kuzingatia muda waliopatiwa.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Senyamule amezungumzia maandalizi ya Mkoa wake kuelekea maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano.

"Tunaelekea maadhimisho ya sherehe ya Muungano tarehe 26/4/2023 na hapa Dodoma tumeanza kuadhimisha toka tarehe 17/4/2023 ambapo tunajivunia mashujaa wetu walioweza kuunganisha Tanganyika na Zanzibar na kuleta Tanzania ambayo hii leo tunajivunia Muungano wenye mshikamano ,usio yumba, wenye mtizamo sahihi kwa wananchi wake wa pande zote mbili na muungano ulio imarika kila sekta kwa Tanzania na Dunia kwa ujumla "Amesema Senyamule

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Jimmy Yonaz amesema fedha za ujenzi zipo tayari na zinatoka kwa wakati ambapo kiasi cha Shilingi bilioni 17 zitatumika kufanikisha ujenzi wa Mnara huo wa mashujaa pamoja na zahanati na sehemu ya kupumzikia na kusisitiza kuwa upande wa usimamizi wamejipanga vizuri .

Nae Meneja wa Kanda wa SUMA JKT Meja Generali Samwel Jambo ambaye pia ndio Mkandarasi wa Ujenzi amesema wamejipanga kutekeleza kazi hiyo kwa wakati na ubora hadi kufikia siku maalumu.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.