• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DKT.MPANGO KUZINDUA MPANGO WA MAKAZI KWA WATUMISHI WA UMMA DODOMA

Imetumwa : December 4th, 2024

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia taasisi yake ya Watumishi Housing Investments (WHI) imeandaa hafla muhimu ya Uzinduzi wa Mpango wa Makazi kwa Watumishi wa Umma utakaozinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango Disemba 11, 2024 katika eneo la Mradi wa Nyumba Njedengwa, jijini Dodoma.

Hayo yamebainishwa leo Disemba 04, 2024 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule wakati akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa ofisi yake iliyopo kwenye jengo la Mkapa Jijini Dodoma.

“Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, inapenda kuwaalika Watanzania wote kushiriki katika hafla hii muhimu ambayo inaashiria hatua kubwa katika kuboresha maisha ya Watumishi wa Umma na maendeleo ya sekta ya makazi Nchini.” Mhe. Senyamule

Aidha, Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji Sera – Ofisi ya Rais Utumishi Bw. Cyrus Kapinga, amesema;

“Siku hiyo utazinduliwa mpango wa Mradi wenye nyumba 206 ambazo zimeshajengwa ambapo nyumba zaidi ya 200 tayari zinatumika pia mahitaji ya nyumba za watumishi ni zaidi ya 200,000 hivyo, kinachofanyika sasa, mpango unalenga kuweka mkakati wa kujenga nyumba nyingi zaidi nchi nzima ili kukabiliana na upungufu wa makazi unaowakabili Watumishi wa Umma.” Bw. Kapinga.

Mpango wa Makazi kwa Watumishi wa Umma ulianza kutekelezwa mwaka 2014 chini ya usimamizi wa WHI na hadi sasa zaidi ya nyumba 1000 zimejengwa katika mikoa 19 nchini ikiwemo Dodoma, Dar es Salaam, Mwanza, Morogoro, Simiyu, na Mtwara ambapo unalenga kuwawezesha Wananchi na hasa Watumishi wa Umma kiuchumi kupitia umiliki wa nyumba.


#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu        

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.