• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DODOMA KUFIKIA ASILIMIA 95 YA UFAULU MWISHONI MWA 2025

Imetumwa : December 17th, 2024

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS

Wakuu wa shule za msingi na sekondari Mkoa wa Dodoma, wametakiwa kutekeleza kikamilifu mpango Mkakati wa elimu kwa kuhakikisha kuwa kufikia mwisho wa mwaka 2025, mkoa unafikia ufaulu wa asilimia 95 kulingana na malengo yaliyowekwa katika mkakati huo

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alipokua akitoa maelekezo wakati wa kikao kazi cha Maafisa elimu Kata, wakuu wa shule na walimu wakuu kilichofanyika katika ukumbi wa Maria De Matias Jijini Dodoma leo Disemba 17, 2024.

Mkuu wa Mkoa, ametoa maelekezo kadhaa ikiwemo kuzingatia utekelezaji wa mpango Mkakati wa elimu kwa miaka mitatu, unaolenga kuinua ufaulu kwa mkoa wa Dodoma.

“Kila Mkuu wa shule, hakikisha unatekeleza mpango Mkakati kikamilifu ili kufikia mwisho wa 2025, Mkoa uwe na ufaulu bora kulingana na malengo tuliyojiwekea katika Mkakati na hapa tumejiwekea malengo ya kufikia 95% ya ufaulu” Mhe. Senyamule

Aidha, Mhe. Senyamule ameagiza upandaji miti katika kila shule hasa miti ya matunda kwani licha ya kivuli, pia itasaidia kupata lishe kwa wanafunzi pamoja na kuongeza kipato kwa shule husika kutokana na kufanya biashara ya matunda.

“Wakuu wa shule za msingi hakikisheni zoezi la upandaji miti linasimamiwa kikamilifu na kila shule ipande miti isiyopungua 500 na kuitunza. Pandeni miti ya matunda kwani ni chakula kwa watoto na itakua ni mradi wa shule kwani mukiamua kuuza matunda mutanunua chakula na itakua ni motisha kwa mapato ya shule.” Mhe. Senyamule

Vilevile, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar Mmuya, amezungumzia suala la motisha kwa walimu kutoka kwa viongozi wao kuwa ni jambo muhimu; “Tuwaone tunaowasimamia kwenye elimu katika eneo lolote kuwa ni wa thamani kwenye nafasi yako ya uongozi, muwapende, muwathamini na muwasikilize”.

Kikao kazi hiki ni muendelezo wa vikao kadhaa vya maafisa elimu, wakuu wa shule na walimu wakuu vyenye lengo la kuboresha na kuhakikisha matokeo bora ya utekelezaji wa Mkakati wa elimu wa miaka mitatu unaosema “Uwajibikaji wangu, ni msingi wa kuinua ubora wa elimu na ufaulu Dodoma” ambayo pia ndio kauli mbiu ya vikao hivyo.


#dodomafahariyawatanzania                                  #keroyakowajibuwangu #mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • DODOMA YADHAMIRIA KUJIKITA KWENYE KILIMO CHA MATUFAHA (APPLES) KUINUA UCHUMI

    May 08, 2025
  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • KAMPUNI YA "CAVO'' YA CHINA YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

    May 05, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.