• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Dodoma kushirikisha JKT na Magereza kuimarisha kilimo na uzalishaji wa chakula kuondoa tatizo la upungufu wa chakula

Imetumwa : September 8th, 2017

Serikali ya Mkoa wa Dodoma imeahidi kushirikiana na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Magereza kwenye shughuli za kilimo kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa chakula kitakachotosheleza mahitaji ya JKT na Magereza kwenye Kambi zao, mahitaji ya chakula kwenye Mkoa wa Dodoma na ziada kupelekwa Serikalini ili kusaidia maeneo Mengine yenye mahitaji.

Mkakati huo umetangazwa Leo Septemba 8, 2017 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Jordan Rugimbana wakati wa sherehe za kuhitimisha mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria operesheni Tanzania ya viwanda ambapo jumla ya vijana 964 wamehitimu mafunzo hayo kwenye kambi ya Jeshi (834 KJ) Makutupora nje kidogo ya Mji wa Dodoma.

Mheshimiwa Rugimbana amesema Mkakati huo wa kuondoa tatizo la upungufu wa chakula Mkoani Dodoma ni utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli la kuhakikisha kila Mkoa unajitosheleza na kujitegemea kwa chakula ambapo ameahidi pamoja na maeneo ya kilimo yanayomilikiwa na Majeshi hayo, Mkoa utaona namna ya kuwaongezea maeneo mengine zaidi kwa ajili ya kilimo.

“Tayari wamejitokeza baadhi ya taasisi ambazo zimekubali kufadhili shughuli za kilimo Mkoani Dodoma na naahidi nitatoa kipaumbele kwa vyombo hivi ili visaidie kuimarisha shughuli za kilimo na uzalishaji wa chakula Mkoani Dodoma” Aliongeza Mheshimiwa Rugimbana.

Aliwataka vijana hao waliohitimu mafunzo ya JKT kuzingatia viapo vyao na kuwa raia wema na mabalozi wa Taifa letu kwa kujiepusha na kupinga vitendo vyote viovu ambapo ameahidi kuwa serikali ya Mkoa wa Dodoma itawapatia vijana hao kipaumbele kwenye kupata ajira mbalimbali kwenye mradi mkubwa wa bomba la mafuta kutoka nchini Uganda hadi Tanga ikizingatiwa kwa Mkoa wa Dodoma bomba hilo litapita kwenye Wilaya mbili (2) za Chemba na Kondoa.

Awali Kamanda Kikosi cha 834 KJ Luteni Kanali Aristide Rutta alibainisha kuwa vijana hao 964 waliohitimu wakiwa kambini hapo wamepatiwa mafunzo mbalimbali yakijumuisha nyanja za Uhodari, Medani, Ukakamavu, Uzalendo, Nidhamu, Uzalishaji kilimo na mafunzo ya darasani yanayojumuisha mambo mengi.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.