• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DODOMA YADHAMIRIA KUFANYA MABADILIKO KWENYE KILIMO

Imetumwa : February 2nd, 2023

DODOMA YADHAMIRIA KUFANYA MABADILIKO KWENYE KILIMO

Maafisa ugani Mkoa wa Dodoma wametakiwa kutumia ujuzi na utaalamu wao walioupata kuhakikisha sekta ya kilimo inainuka na kufanya mabadiliko makubwa kwenye Mkoa. Hayo yamebainishwa wakati wa kikao kazi kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule alipokuwa akiongea na maafisa ugani kutoka Halmashauri zote nane za Mkoa wa Dodoma kwenye ukumbi wa shule ya Maria de Mathias eneo la Kisasa Jijini Dodoma. Mhe. Senyamule

amewaambia Maafisa ugani hao kuwa Mkoa umedhamiria kufanya Mapinduzi makubwa kwenye Kilimo kutokana na Serikali ya Awamu ya Sita kuonyesha dhamira kwenye sekta hiyo."Dodoma tunataka kufanya mapinduzi makubwa kwenye Kilimo na Rais wetu ameshaanzisha hilo kwa kutujengea mabwawa ya umwagiliaji katika Wilaya za Chamwino na Mpwapwa. Matarajio ya Serikali ni Tanzania kuwa kitovu cha kilimo Afrika" Amesema Mh. Senyamule Ameongeza

kuwa lengo la Mkoa ni kilimo kuwa na tija kwa kuwa wataalamu wa kutosha wapo."Tunataka kilimo cha Mkoa wa Dodoma kiwe na tija kwa Mkoa na nchi kwa ujumla. Haihitaji mabilioni kufanya mabadiliko, kila Afisa ugani awe na shamba darasa lake kwani ni wajibu wenu kuwaelekeza wananchi hatua za kilimo bora kwa mifano hai kutoka kwenye mashamba yenu" Mhe. Senyamule.

Kadhalika, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatuma Mganga, amesisitiza kuwa suala la umaskinj kwenye Mkoa wa Dodoma linatokana na Kilimo kutopewa kipaumbele."Suala la kilimo halijapewa uzito wa kutosha, tunayo ardhi ya kutosha, ni muhimu tufanye mabadiliko na mageuzi ya kimkakati ili tuondokane na umasikini. Kilimo hakipewi msisitizo kama elimu, asiyelima hachukuliwi hatua yeyote. Bila kufufua kilimo, hatuwezi kufufua elimu, afya na sekta nyingine kwani kilimo ndio Mama anayetegemewa kuendeleza sekta nyingine. Hatuwezi kuondoa umaskini bila kufanya mageuzi kwenye Kilimo" Amesisitiza Dkt. Mganga

Akiwasilisha taarifa ya sekta ya kilimo kwenye mkutano huo, Afisa Kilimo Mkoa Bw. Abraham Benard amesisitiza matumizi ya mbolea kwenye Kilimo kwa kutoa takwimu juu ya wakulima wanaotumia mbolea kuwa, hadi kufikia Januari 30, 2023 jumla ya wakulima 2,221 walifanikiwa kununua mbolea ya ruzuku kati ya wakulima 107,994 walioandikishwa na wenye sifa ya kununua sawa na asilimia 2.1

Kikao hicho pia kimeweka maazimio kadhaa kwa lengo la kuinua sekta hiyo kwa mwaka huu ikiwa ni pamoja na; kila Kaya kulima ekari moja ya alizeti, 1 ya mtama na 1 ya zao jingine ili kupata soko la kutosha, Maafisa ugani kuwa na malengo na kuyatekeleza, matumizi ya TEHAMA kwa maafisa ugani kufikisha taarifa kwa wakati, kuwepo kwa mpango kazi wa Mkoa kwa maafisa ugani wote na Kuazimia maafisa ugani wote kuwa wabunifu na kuwa na dhamira ya dhati katika kusuma mbele agenda ya kilimo nchini. MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2020 January 15, 2021
  • MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2020 January 15, 2021
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021 SHULE ZA BWENI (WASICHANA NA WANAUME) . December 20, 2020
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA YA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2020 January 15, 2021
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KATIBU TAWALA SINGIDA AKABIDHI OFISI KWA KATIBU TAWALA DODOMA

    March 23, 2023
  • MACHINGA DODOMA WAMPONGEZA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

    March 23, 2023
  • KIWANDA CHA AINA YAKE KUJENGWA KONGWA

    March 17, 2023
  • WAFANYAKAZI WAASWA MSHIKAMANO MAHALA PA KAZI

    March 15, 2023
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Mkoa akiongoza siku ya maombi jijini Dodoma
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.