• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DUWASA YAJIPAMBANUA UHAKIKA WA MAJI DODOMA

Imetumwa : February 28th, 2023


Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira Mkoa wa Dodoma (DUWASA) inaendelea kufanikisha lengo la upatikanaji wa maji kwa asilimia 100 kwa Mkoa wa Dodoma kufuatia juhudi za Serikali ya awamu ya Sita. Hayo yamebainishwa wakati wa mfululizo wa vipindi maalumu vya kutangaza mafanikio ya Serikali kwa Taasisi za Umma vilivyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambapo leo kimeangazia sekta ya maji.

Akiwasilisha hotuba yake mbele ya wanahabari wakati wa utangulizi wa kipindi hicho, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameelezea miradi mbalimbali ya maji inayoendelea katika Mkoa na utekelezaji wake ndani ya kipindi hiki cha miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita.

“Tunafahamu maji ni kila kitu katika maisha ya mwanadamu, maji ni Uhai. Katika Mkoa wa Dodoma, kumekuwa na Uendelezaji wa vyanzo vya maji (uchimbaji wa visima na ujenzi wa mabwawa) kwa kutumia vyanzo vikuu kama vile Uchimbaji wa visima  virefu 34, Ujenzi wa Mabwawa 2 ya maji, miradi 10 ya maji inayotumia mtandao wa bomba imekamilika, Uzalishaji wa Maji umeongezeka kutoka wastani wa lita 61.5 Milioni hadi lita 67.8 Milioni. Ongezeko hili la uzalishaji limetokana na kukamilika kwa Miradi Mipya ya Maji yenye thamani ya Shilingi 9.14 Bilioni. Upatikanaji wa huduma ya Maji vijijini kwa Mkoa wa Dodoma umefikia wakazi 1,393,167 sawa na asilimia 65.1 na Lengo la Serikali ni kuhakikisha tunamtua Mama Ndoo kichwani miradi ya maji inaendelea kila Wilaya ili kufikia 85% ya upatikanaji wa maji vijijini ifikapo 2025” Amesema Mhe. Senyamule

Akifafanua mipango ya muda mrefu na wa kati ya Serikali kwa Mamlaka hiyo juu ya kuhakikisha upatikanaji wa maji unakua wa uhakika kwa Mkoa wa Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo Mhandisi. Aron Joseph amesema;

“Serikali ina mipango ya kati ya kuhakikisha inamaliza tatizo la upatikanaji wa maji ikiwemo mradi wa Bwawa la Farkwa katika Halmashauri ya Chemba unaogharimu kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 793.5, mradi wa kutoa maji kutoka Ziwa Victoria ambapo upo katika hatua ya usanifu. Pia kuna mpango wa dharura wa kuchukua maji kutoka Bwawa la Mtera lita Milioni 130 kwa siku sawa na asilimia moja ya maji yanayozalisha umeme ambayo yatasambazwa Dodoma nzima na mradi huu utagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 326” Amesema Mhandisi. Aron

Vilevile Mkurugenzi huyo ameainisha baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo katika utendaji wao wa kazi ikiwemo wizi wa miundombinu ya maji taka hasa mifuniko, wananchi kutupa taka ngumu kwenye mabomba ya maji taka hali inayopelekea mifereji kuziba na kusababisha kero ya kuvuja kwa maji taka kwenye makazi ya watu, wananchi kutozingatia matumizi sahihi ya maji safi hali inayopelekea upotevu wa maji, wanachi kutopenda kusoma taarifa za maji na kusababisha kero wakati wa kulipa bili, wizi wa maji pamoja na mita.

DUWASA ina matarajio makubwa kufikia mwaka 2025 ikiwemo kukamilika kwa miradi yote inayoendelea hivi sasa ili kutimiza lengo la Serikali ya Awamu ya sita kwa Makao makuu ya nchi kwani Serikali imehamia Dodoma na bado viongozi wanaendelea kuhamia kwa awamu tofauti hivyo ni lazima miundombinu ya maji iwe ya uhakika na thabiti ili kuweza pia kuvutia wageni wakiwemo wawekezaji wanaoingia kwa wingi katika Mkoa huu.

MWISHO

                                          

                                 

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.