• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA YATOA MIKOPO YENYE THAMANI NYA TSH.1.38 BLN

Imetumwa : November 2nd, 2022

Halmashauri ya Jiji la Dodoma imekabidhi mfano wa hundi ya mikopo ya asilimia 10 kwa makundi maalum ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kama sheria ya manunuzi ya Serikali inavyozitaka Halmashauri zote kufanya hivyo. Hafla hiyo imefanyika kwenye viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amehudhuria kama mgeni rasmi.

Katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa amesema kuwa, hii ni mara ya kwanza kwa fedha nyingi kutolewa kwa wajasiriamali na amewapongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kutimiza na kutekeleza sheria hii

“Nitoe pongezi sana kwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwani mumeonyesha njia kwa kuwa wa kwanza kutekeleza sheria hii. Halmashauri nyingine mujipange nanyi kuhakikisha munatekeleza hili. Hii ni dhamira ya dhati ya Mhe. Rais kuhakikisha wafanyabiashara wasio na uwezo wa kukopa kwenye Taasisi kubwa kama Benki, wanafaidika kwa mikopo hii nafuu na isiyo na riba kutoka Serikalini” RC Senyamule.

Mkuu wa Mkoa pia ametoa wito kwa wajasiriamali hao kutumia mikopo hiyo kwa uaminiifu ili waweze kuirudisha kwa wakati ili iwasaidie na wengine.

“Fedha hii sio zawadi, ni mkopo, inatakiwa kulipwa na isiporudishwa itapelekea kutungwa kwa sheria ngumu. Tukafanye kazi turudishe mikopo ili na wengine waweze kupata. Kila anayepewa fedha hizi aziheshimu, asizichezee” Ameongeza

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Bw. Joseph Mafuru, akitoa mchanganuo wa fedha hiyo kiasi cha Shilingi Bilioni 1.38 zilizogawiwa kwa makundi maalum ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

“Katika kipindi cha Julai hadi Septemba, Halmashauri ya Jiji ilipokea maombi ya mikopo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 5.83 kutoka katika vikundi 102 vilivyoidhinishwa. Mchanganuo wa mikopo hii ni kama ifuatavyo; vikundi 46 vya wanawake vimepata Shilingi Milioni 500, vikundi 33 vya vijana vimepata Shilingi Milioni 693 na vikundi 23 vya walemavu vimepata Shilingi Milioni 195.25 Mkopo huu umetoa Shilingi Milioni 467.48 kutoka kwenye mapato ya ndani ya Halmashauri na Shilingi Milioni 922.07 kutoka kwenye marejesho ya mikopo iliyotolewa awali” Bw. Mafuru

Hata hivyo, Naibu Meya wa Jiji la Dodoma, Bw. Jamal Yaredi amewasisitiza wafanyabiashara kuitumia mikopo hii kwa umakini ili waweze kuirudisha kwa wakati na iweze kuwasaidia wengine mwaka ujao. Pia amewaasa kuitumia vizuri ili iweze kuleta tija kwa biashara zao ziweze kukua na pamoja na kuwa msaada kwa familia zao.MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2020 January 15, 2021
  • MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2020 January 15, 2021
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021 SHULE ZA BWENI (WASICHANA NA WANAUME) . December 20, 2020
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA YA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2020 January 15, 2021
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • SENYAMULE AAGIZA UJENZI WA MADARASA KUKAMILIKA KWA WAKATI

    May 29, 2023
  • CHEMBA WAASWA KUTOFANYA KAZI KWA MAZOEA

    May 27, 2023
  • GUGU AKUTANA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA CAMBRIDGE

    May 23, 2023
  • SENYAMULE AZINDUA JUKWAA LA PILI LA VYAMA VYA USHIRIKA

    May 19, 2023
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Mkoa akiongoza siku ya maombi jijini Dodoma
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.