• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

"HUDUMA SIO DAWA, MGANGA PAMOJA NA MUUGUZI,HUDUMA NI PAMOJA NA MWONEKANO WENU" DKT.FATUMA MGANGA MAZINGIRA,UKARIMU NA

Imetumwa : October 13th, 2022

Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatuma Mganga, ameyasema hayo wakati ametembelea Hospitali na vituo mbalimbali vya huduma za afya vya Mkoa wa Dodoma ikiwemo kituo cha afya cha Makole. Lengo la ziara hiyo ni kukagua dawa pamoja na vifaa tiba.

Akiwa katika kituo hicho, baada ya kukagua dawa pamoja na vifaa tiba, Dkt. Mganga ametembelea na  kukagua wodi zinazopatikana kituoni hapo ikiwemo wodi ya wazazi, chumba cha maabara na vingine vinavyohusika na utoaji wa huduma za afya  kwa wananchi.

Baada ya ukaguzi huo, Katibu Tawala Mkoa ameongea na baadhi ya watumishi wa afya wanaohudumia kituo hicho wakiongozwa na Mganga mkuu wa kituo, viongozi wa idara pamoja na watumishi wote kwa pamoja.

Katibu Tawala Mkoa Dkt. Fatuma Mganga ameongelea suala kubwa la ukiukwaji wa maadili kwa wahudumu wa afya ikiwemo kutoa huduma tofauti na ugonjwa, kauli chafu kwa wagonjwa, wizi wa dawa za wagonjwa nk.“Nimekua nikipata simu kutoka kwa wagonjwa wakilalamika kwamba wapo hapa lakini hakuna wahudumu, niwaambie tu kwamba kazi ya kutoa huduma kwa wananchi hasa huduma za afya ni nyeti sana na sio sawa na kazi yoyote ile kwani hapa tunashughulika na uhai wa mwanadamu”

“Kuna baadhi ya wahudumu hawatumii nafasi zao vizuri kwa kutoa huduma mbovu kwa wagonjwa kinyume na maadili ya taaluma hii. Tutumie vizuri neema hii tuliyopewa ya kupata ajira kwani kuna wengi wamesoma lakini hawajabahatika kupata ajira” amesema.

Kadhalika, Dkt. Mganga amewaambia wahudumu hao kuwa Serikali inafanya jitihada kuboresha sekta ya afya kwa kujenga majengo ya huduma pamoja na kuleta vifaa tiba na kituo cha Afya Makole kimepata Shilingi Milioni 750 kwa ajili ya kuboresha majengo ya Kituo hiki

“Fedha hizi mlizopata zinaweza kujenga jengo zuri la ghorofa hapa pakapendeza, lakini uzuri wa jengo usio na watumishi wenye huduma bora, linapoteza maana ila jengo likiendana na huduma bora inakua ni kitu chema”

Hata hivyo, Dkt.Mganga amewataka watumishi hao kuhakikisha wanakua na tabia njema kwani kazi hii ni ya maadili na ina taratibu zake ambazo zinamfanya mgonjwa kuwa huru kuelezea tatizo lake kwa Mganga lakini inapokua tofauti atashindwa kuelezea tatizo lake kwa hofu.

“nina wajibu wa kuwaeleza haya kwani ndio kazi yangu, huduma sio dawa tu na mganga pamoja na muuguzi, huduma ni pamoja na mazingira, ukarimu na muonekano wetu. Wagonjwa wanategemea tuwaonyeshe huruma ya hali ya juu, hii ni kazi ya kupokea baraka au laana hivyo nawaomba tupokee baraka hizi za bure kwa nafasi hizi tulizopata maana ukifanya jambo la kupokea laana, hiyo itakua ya kwako” . Amesisitiza Dkt. Mganga.

MWISHO

 

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2020 January 15, 2021
  • MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2020 January 15, 2021
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021 SHULE ZA BWENI (WASICHANA NA WANAUME) . December 20, 2020
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA YA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2020 January 15, 2021
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KATIBU TAWALA SINGIDA AKABIDHI OFISI KWA KATIBU TAWALA DODOMA

    March 23, 2023
  • MACHINGA DODOMA WAMPONGEZA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

    March 23, 2023
  • KIWANDA CHA AINA YAKE KUJENGWA KONGWA

    March 17, 2023
  • WAFANYAKAZI WAASWA MSHIKAMANO MAHALA PA KAZI

    March 15, 2023
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Mkoa akiongoza siku ya maombi jijini Dodoma
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.