• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KAMILISHENI UJENZI KWA WAKATI - SENYAMULE

Imetumwa : July 30th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule  ameagiza wakandarasi wanaotekeleza mradi wa ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Mpwayungu iliyopo Wilayani Chamwino kukamilisha michoro ya ujenzi huo ili kuwezesha kazi nyingine kuendelea.

Mhe. Senyamule ametoa agizo hilo mwishoni mwa wiki wakati wa ziara yake ya kikazi katika Wilaya hiyo katika Kata ya Mpwayungu ambapo ametembelea miradi kadhaa ikiwemo Ujenzi wa Shule hiyo, Mradi wa kupambana na Ujangili na biashara haramu ya Wanyamapori katika mfumo wa ikolojia wa hifadhi za Ruaha [WMA] katika kijiji cha Ndogowe na Mradi wa Kilimo cha Pamoja (BBT)

Amesema kuwa iwapo michoro hiyo itakamilika kwa wakati itatoa fursa kwa wananchi kuendelea na zoezi la kuchimba msingi ndani ya wiki moja.

Mhe. Senyamule ameelekeza Watendaji kuhakikisha wanasimamia kazi zinazo wahusu ikiwemo Uchimbaji wa msingi, kusogeza kokote ,vifusi vya mchanga ili mradi huo uweze kwenda kasi na kukamilika kwa wakati.

" Natarajia kuona uchimbaji wa msingi umekamilika ndani ya siku saba na kufanya hivyo ni ishara ya kwamba mnauhitaji wa uharaka wa maendeleo kwani serikali inahitaji kasi na ufanisi" ameeleza Senyamule

Aidha amesema kuwa kiasi cha Fedha zaidi ya Shilingi milioni 544 zimeshatolewa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo japo kasi ya utekelezaji ni ndogo, hivyo ametoa rai kuongeza kasi ili ifikapo tarehe10/10/2023 mradi uwe umekamilika.

 

Mradi huo unahusisha Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa 8, Jengo la Utawala , Maktab, Chumba cha Tehama ,Matundu ya vyoo vya wanafunzi 8, Maabara ya Sayansi 3, Tanki la Kuhifadhia maji moja la Lita 32000 , Kichomea taka na jenereta vinavyotekelezwa chini ya ufadhili wa Fedha za SEQUIP.

Katika hatua nyingine Mhe. Senyamule akiwa kwenye Mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Mlazo na Ndogowe amesisitiza wananchi kujitokeza kushiriki kwa kutoa nguvu kazi kwenye ujenzi wa Shule ya Sekondari Mpwayungu

"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan ameelekeza kila Kata kuwa na Shule ya Sekondari amefanya jitihada na anaendelea kutupatia fedha kwa ajili ya kutengeneza Miundombinu wezeshi kwa watoto ili maendeleo ya mguse kila mmoja hivyo tushirikiane kuunga mkono jitihada hizo." Ametoa wito Mhe. Senyamule

Hata hivyo, Mhe.Senyamule amekemea vikali suala la Utoro wa watoto Shuleni na hatua kali za kisheria kuchukuliwa kwa wazazi wazembe kufutilia mienendo ya watoto wao na wengine wanaobaki nyumbani kwa ajili ya shughuli za nyumbani na hivyo kupelekea watoto hao kuto maliza masomo.

"Tutafutilia lazima tutahakikisha mtoto mmoja mmoja anapata haki yake ya msingi ya kupata Elimu na kuwachukulia hatua kali kwa wazazi watakao bainika wanachangia watoto wao kuwa watoro Shuleni "amesisitiza Senyamule

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Gift Msuya amesema kuwa ujenzi wa Shule hiyo umezingatia vigezo vyote ikiwemo umbali kwa wanafunzi na kuwataka wakazi wa kata hiyo kubadilika kwani maendeleo hayajaribiwi washirikiane ili kusogea mbali kuitekeleza kesho .

Kwa upande wake Afisa Elimu wa Mkoa wa Dodoma Mwl. Gift Kyando amewataka

wakandarasi wanaohusika na Ujenzi wa Shule hio kutoharibu mazingira kwa kukata miti ovyo .

Mwalimu Kyando ametoa wito kwa wakazi wa eneo hilo kutoa ushirikiano pindi ujenzi unavyoanza sambamba na kutumia fursa zilipo kwa muda wa utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa katika Kata hiyo.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.