• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KONDOA MJI YATOA SHILINGI MILIONI 193 MIKOPO YA ASILIMIA 10

Imetumwa : November 13th, 2024

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS

Halmashauri ya Kondoa Mji katika Wilaya ya Kondoa, Mkoa wa Dodoma, imetoa jumla ya shilingi milioni 193 ikiwa ni mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Hafla ya utoaji wa mikopo hiyo imefanyika Novemba 13, 2024 katika Kata ya Bicha na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alipofanya ziara katika Wilaya hiyo ambapo kikundi cha vijana Bicha, kimenunua pikipiki tano kwa wana kikundi.

“Kwa kutekeleza maelekezo ya Mhe Rais wetu ya kutoa 10% kwa makundi maalumu, Halmashauri ya Kondoa ndio ya kwanza kutoa mikopo hii. Nisisitize, kabla ya mwezi huu haujaisha, lazima wawe wametoa hela hizo. Nyinyi muliopata mikopo msifikiri ni jambo dogo”. Amesema Mhe. Senyamule

Awali, kabla ya kumkaribisha Mhe. Senyamule, Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Fatma Nyangasa, amesema mikopo hiyo imetolewa kwa awamu ya kwanza lakini bado itatolewa zaidi.

“ Kwa awamu ya kwanza Halmashauri yetu ya Kondoa Mji imetoa shilingi Milioni 193 kwa ajili ya vikundi hivi vya Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu. Tayari wamekwisha pokea, lakini kuna zaidi ya shilingi Milioni 100 nyingine ambayo ipo tayari kwa ajili ya kulipa vikundi vingine vinavyoendelea.” Mhe. Nyangasa

Licha ya kuhudhuria hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma pia alitembelea na kukagua ujenzi wa madarasa 4 kwa gharama ya shilingi 92,000,000 na matundu 8 ya vyoo (14,400,000) katika shule ya Sekondari Dilai ambao upo kwenye hatua ya umaliziaji.

Miradi mingine iliyo kaguliwa ni shule mpya ya Mafunzo ya Amali Kingale unaogharimu shilingi 544,225,626 pamoja na ujenzi wa madarasa mawili na mabweni mawili kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha tano (2025/2026) katika shule ya Sekondari Bukulu unaotekelezwa kupitia programu ya SEQUIP kwa shilingi 296,000,000.


#kurayakosautiyako              

#ujanjanikupigakura              

#dodomatukotayarikupigakura

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.