• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KONGWA YAJIVUNIA KITUO CHA UMAHIRI CHA MAZAO - MTANANA

Imetumwa : March 10th, 2023

Wilaya ya Kongwa ni miongoni mwa Wilaya saba zinazounda Mkoa wa Dodoma inayojivunia mafanikio kadha wa kadha yaliyopatikana katika sekta mbalimbali ndani ya kipindi cha miaka miwili tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mafanikio ya Wilaya hiyo yameelezwa wakati wa kipindi mubashara cha kutangaza mafanikio ya Mkoa wa Dodoma kwa Taasisi za umma kilichorushwa mwishoni mwa wiki.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amesema kwa Wilaya ya Kongwa, Serikali imefanikiwa kutoa fedha za ujenzi wa kituo Mahiri cha mafunzo kwa wakulima katika eneo la Mtanana

“Wana Dodoma wana furaha sana na kuishukuru Serikali kwa utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Kituo Mahiri cha Mafunzo kwa wakulima na usimamizi wa Mazao baada ya mavuno Mtanana – Kongwa. Hiki ni kituo cha kipekee na cha mfano kwa Afrika Mashariki, kitakuwa na utaalamu wa kuzuia sumu kuvu kwenye mazao na kitawezesha mazao yetu kuuzika kimataifa. Mradi huu upo chini ya Wizara ya Kilimo na unagharimu takribani kiasi cha shilingi Bilioni 19 huku ujenzi wake ukitarajiwa kukamilika Oktoba 2023. Mradi huu ni wa kimkakati ambao utasaidia usimamizi endelevu wa mazao” Amesema Mhe. Senyamule

Aidha, Mradi huu unatarajiwa kuwanufaisha wakazi wa Dodoma kwani utasaidia upatikanaji wa ajira kwa wananchi na kwa namna ya kipekee mradi huu unaifaharisha na kuistawisha Dodoma kwa namna yake.

Kama ilivyo ada, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kongwa Dkt. Omary Nkullo, amedadavua kwa undani mafanikio katika sekta ya nishati ambapo amesema kuwa;

“Vijiji vilivyounganishwa na huduma ya umeme vimeongezeka kutoka Vijiji 63 mwaka 2021 hadi kufikia Vijiji 83 mwaka 2022 sawa na ongezeko la asilimia 95 ya vijiji vyote vya Wilaya. Wilaya inaendelea na utekelezaji wa mradi wa REA awamu ya III, mzunguko wa pili kwa thamani ya shilingi Bilioni 39 katika vijiji vya Makutupa, Silale, Suwi, Vilundilo, Lobilo, Silwa na Saigoni.

Hata hivyo, kupitia mradi wa Peri Urban unaotekelezwa na Mkandarasi Ceylex Engineering Co. Ltd kwa thamani ya shilingi Bilioni 17.3, Vitongoji sita katika Mamlaka ya Mji mdogo wa Kibaigwa, eneo moja Kijiji cha Mbande na Vitongoji Viwili katika Kijiji cha Laikala, vimepata huduma ya umeme. Ukarabati wa miundombinu mbalimbali ya umeme ikiwa ni pamoja na uwekaji wa nguzo za zege katika maeneo korofi na mengine yaliyopewa kipaombele. Jumla ya shilingi Milioni 617,249,594.35 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji na utekelezaji huo unaendelea” Amefafanua Dkt. Nkullo

Mkurugenzi huyo pia amegusia mafanikio yaliyopatikana kwenye sekta ya miundombinu ambapo amesema kuwa Wilaya ina mtandao wa barabara wenye jumla ya Km 1213.45. Barabara za Wilaya zinapitika kwa wastani wa 55% katika kipindi chote cha mwaka. Kiwango cha 35% zinapitika kwa shida kipindi cha mvua na 10% hazipitiki kabisa. Barabara za changarawe zimeongezeka kwa 24.34%, barabara za udongo zimepungua kwa 16.79% huku ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami zikiongezeka kutoka Km 3.7 hadi kufikia Km 8.7 Barabara hizi zimesaidia kukua kwa Mamlaka za Miji midogo ya Kongwa na Kibaigwa na kuongezeka kwa shughuli za kibiashara katika mitaa.

MWISHO

 

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.