• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KONGWA YAPONGEZWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

Imetumwa : November 14th, 2023

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma Bi. Pilli Mbaga amepongeza Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo  katika Wilaya ya Kongwa Novemba 14, 2023 ikiwa ni siku ya pili ya ziara ya ukaguzi wa miradi inayotekelezwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Wilayani humo.

Katika ziara hiyo  kamati ya Siasa ya Mkoa imetembelea na kukagua miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa Barabara ya kiwango Cha Lami ya Mwalimu Nyerere yenye urefu wa Km 1  Kwa thamani ya Shilingi 487,199,000.00 kutoka mfuko wa Jimbo wa Barabara ,  Ujenzi wa Miundombinu katika Hospitali ya Wilaya wenye thamani ya Shilingi Bilioni 4.64 unaohusisha Wodi tatu za wagonjwa na Jengo la mama na mtoto.

Miradi mingine ni Ile ya Kisima cha Maji katika Kijiji Cha Laikala "B" wenye thamani ya Shilingi 780,566,436.64  Shule ya Msingi Moleti iliyojengwa kupitia mradi wa BOOST Kwa thamani ya Shilingi  318,800,000.00 na mradi wa Kuboresha umeme Kwa ajili ya kutatua kero ya umeme hafifu Kwa Wilaya za Kongwa Mpwapwa na Gairo, unaohusisha ujenzi wa njia ya msongo wa Kilovoti 33 kutokea kituo kidogo Cha Zuzu hadi Mbande wenye thamani ya Shilingi 5,104,849,344.90.

Aidha, katika miradi yote hiyo Kamati imetoa Pongezi za dhati na kutoa Rai Kwa Wananchi kuendelea kuiamini Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais wake Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,  kwani imedhamiria kutatua kero zinazowakabili Wananchi.

Akipongeza Mradi wa ujenzi wa Miundombinu katika Hospitali ya Wilaya Bi. Mbaga amewataka Madaktari na Wauguzi kuwa na kauli nzuri Kwa Wagonjwa Ili kutimiza dhamira nzuri ya Serikali ya kutoa huduma bora kwa wananchi wake.

Akizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa ziara hiyo, Mbunge wa Jimbo la Kongwa na Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai, pamoja na kushukuru jitihada za Serikali za kuwaletea Wananchi Maendeleo, pia ametoa wito Kwa Serikali Kuboresha taratibu zake katika kuhudumia Wananchi ikiwemo kutenga Fedha zinazojitosheleza kutekeleza Miradi mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya wananchi. Aidha Mhe. Ndugai amesikitishwa na kero ya kukatika Kwa umeme mara kwa mara hali inayopelekea kurudisha nyuma jitihada za Wananchi katika kujiletea Maendeleo kupitia viwanda mbalimbali vya uzalishaji.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.