• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

" Kutatua Migogoro Sugu ya Ardhi Dodoma, Azisheni Kanda za Ardhi" RC- Mtaka

Imetumwa : July 6th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Antony Mtaka ameagiza kuanzishwa kwa kanda za ardhi (zones) ili kuondoa migogoro ya ardhi huku akiwataka wataalam wa Ardhi waliohamishiwa Mkoani Dodoma kufanya kazi kwa weledi.Mhe Mtaka ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao na Watumishi wa Idara ya Ardhi jiji la Dodoma na Ofisi ya Kamishna wa Ardhi msaidizi Mkoa wa Dodoma.

Mkuu wa Mkoa amesema kuwa kuna umuhimu wa kuanzisha kwa kanda za ardhi zitakazosaidia kuondoa migogoro ya ardhi ambayo imekuwa mingi huku kukiwa na taarifa za baadhi ya Wakuu wa mikoa,Wilaya na viongozi mbalimbali licha ya kuwa na hati za umiliki lakini maeneo yao yamemilikishwa kwa watu wengine.

Mhe. Mtaka amesema makosa ya nyuma ambayo yamesababisha utwaaji wa ardhi ulioleta malalamiko, yasijirudie na wataalam wa ardhi wasiwe sehemu ya mgogoro wa ardhi. "Tuwatambue wamiliki wote wa ardhi na tuilinde.Migogoro yote iwe kidigital, ili isiwe mipya sababu ya viongozi wapya na wakati mwingine migogoro mingi ni sababu ya sisi viongozi wenyewe,"  amesema Mhe.Mtaka.

Mhe.Mtaka amesema, kuwa kiongozi inamaanisha kufanya maamuzi, kasikilizeni wananchi vizuri. Hiki kikao ni cha mafunzo , pia tunataka tutatue migogoro , Sasa timu imebadilshwa. Aidha Mhe.Mtaka amewataka wataalam 10 wa Ardhi waliohamishiwa Dodoma kufanya Kazi kwa weledi ili kwa pamoja waweze kutatua migogoro ya ardhi. "Timu mpya ya wataalam wa Ardhi  imeripoti kuja kufanya Kazi Dodoma  fanyeni kazi kwa weledi Ili kuondoa migogoro ya ardhi Ili siku Moja Waziri wa Ardhi aone ameleta watu sahihi,"amesisitiza Mhe. Mtaka.

Aidha, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatuma Mganga amesema Jiji la Dodoma linaongoza Kwa migogoro nchini."Asilimia 90 ya wanainchi wanaokuja ofisini kwetu ni malalamiko ya ardhi. Hivyo Mkurugenzi, ni vyema maeneo ya migogoro mkawagawiwa hawa watumishi wapya kwenye zones na kila mmoja apewe zone yake/Eneo lake na amilikishe migogoro yote na kutatua migogoro hiyo. Watumishi hawa wapimwe kwa idadi ya migogoro waliyoitatua.Masuala ya migogoro yawe agenda mtambuka kwenye kila kikao na taarifa itolewe." Amesema Dkt. Mganga.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri ametaka kuwekwa kwa mpango kazi na mgawanyo wa majukumu."Tukiweza kwenye teknolojia hawa watu 45 tutawasimamia vizuri tu. Dodoma pana kazi nyingi sana, tuna zao la zabibu, zao la zabibu ni zao kipaumbele Kwa Serikali ya Tanzania. Kwenye kila Mikoa yetu kuna zao la uchumi ambalo linasaidia mkoa wowote kupaa. Tusijaribu kubomoa mashamba ya zabibu.Upimaji wa viwanja uwe wa huruma zaidi badala ya kufikiria kuongeza kipato".Amesema Mhe. Shekimweli.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Mhe. Joseph Mafuru  amesema " Wizara ya ardhi watusaidie, maana tuna kilio  cha control namba.Suala la  control namba na hati ni  muhimu sana bila ya hivyo ni kasheshe. Kamishna na Wizara title na control number vipewe kipaumbele, Mteja wa kwanza awe wa kwanza kupata huduma yaani ‘FIRST IN FIRST OUT’ (FIFO) utaratibu huo ndio utumike.Na ifanyike  bila kuangalia cheo wala wadhifa.“Wale wenyeji msiwachomekee wageni." Amesema Mhe. Mafuru.

“Makampuni yanahongeka. Hatujitaji tena makampuni ya kupima.Tutatumia wataalam wa ndani. Kwani tayari tumeeshanunua vifaa  vyenye thamani ya Tsh.Tsh.246 mln ambavyo ni vifaa vya survey, tumenunua magari 3 Kwa ajili ya upimaji.Ukipokea kazi  ya mtu yeyote heshima ni kuikamilisha." Amesisitiza Mhe. Mafuru.

Kamishna Msaidizi wa ardhi Mkoa wa Dodoma, Bw. Thade Ardo Kabonge ameeleza chanzo  kikubwa cha kuongezeka  kwa migogoro ni  wingi wa madalali ambao wanatutmia sisi bila kujijua. Hivyo mtumishi wa ardhi unaposhighulikia mgogoro jihakikish huyo unayeshughulika nae ndie mmiliki halali wa kiwanja.

 Akizungumza Katibu Tawala Msaidizi Miundo mbinu- Mhandisi. Happiness Mgalula amesema kuwa, Dodoma ndio Makao Makuu ya nchi mkifanya kazi vizuri mtaonekana tu. "Kwa wananchi wenye matatizo ya zamani, ni vyema kufanya uchunguzi, tuwape wananchi majibu ya staha  na tuwaonyeshe tunawaheshimu utakuta mtu anakuja kupata huduma kabla hajatoka umeshaanza kumkejeli," hilo si jambo jema.Unapotoa huduma kwa  mwananchi hakikisha upo sawa huna hasira. Wananchi waelimishwe kuhusu utaratibu mpya, ofisi nzima lazima wajue hiyo program ili Mwananchi akija kila Mtumishi awe na uwezo kwa kujibu kwa ufasaha ili mwananchi apewe jibu sahihi na kwa wakati, usimsengenye mwananchi" amesisitiza Mhandisi Mgalula.

Meya wa Jiji la Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe amesema uhamisho umefanyika ili kuondoa wale wote wenye kuleta ukakasi.”Mwananchi kutokusikilizwa hiyo kwake ni dhuruma.Lugha ya faili halionekani nalo ni tatizo na hatua zichukuliwe.Maafisa jengeni ujasiri na kujiamini.Faraja ya kazi ipatikane Kwa huduma mnayotoa Kwa wananchi na sio kwa kile mnachokipata.Mkurugenzi wapime watu wako Kwa Huduma walizotoa."  Amesema Profesa Mwamfupe.

MWISHO.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC SENYAMULE AFUNGUA MAADHIMISHO YA KITAIFA YA SIKU YA NYUKI DUNIANI

    May 18, 2025
  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.