• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Kwa Ufupi Yaliyojiri kwenye Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dodoma Jumamosi Disemba 23, 2017

Imetumwa : December 28th, 2017

KWA UFUPI YALIYOJIRI KWENYE KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA DODOMA JUMAMOSI DISEMBA 23, 2017

Chini ya uenyekiti wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge, Kamati ilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Mkoa wakiwemo Wabunge wa Mkoa wa Dodoma wakiongozwa na Spika wa Bunge la Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai ambaye ni Mbunge wa Kongwa, Viongozi wa Wilaya zote za Dodoma, Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dodoma, Maafisa wa Sekretarieti ya Mkoa na Wadau mbalimbali wa Maendeleo.

Uboreshaji Elimu na Kiwango cha Ufaulu

•Bado hali ya ufaulu wa elimu ya msingi na sekondari kidato cha nne kwenye Mkoa wa Dodoma sio ya kuridhisha, sio nzuri

•Kamati iliagiza Wilaya ziitishe Mikutano ya wadau wa Elimu kujadili mikakati ya namna ya kuboresha Elimu na kiwango cha ufaulu kama kuboresha Miundombinu, utoaji chakula mashuleni kwa wanafunzi, Mgawanyo wa Walimu nk.

•Kamati pia ilimuagiza Katibu Tawala wa Mkoa pia kuitisha kikao cha Wadau wa Elimu wa Mkoa baada ya Vikao vya Wilayani kufanyika, lengo kujadili mikakati ya kuboresha kiwango cha Elimu na ufaulu kwenye Mkoa wa Dodoma.

•Katika kuboresha na kujenga miundombinu mipya ya Elimu, Kamati ilielekeza kila Wilaya kuainisha mahitaji yake yote ya vifaa kwa ajili ya ujenzi na kufanya utaratibu wa kununua kwa pamoja kutoka viwandani baada ya taratibu zote muhimu kufuatwa, lengo kupunguza gharama ya ujenzi wa miundombinu.

•Kamati ilitaka Mkoa kupitia Katibu Tawala wa Mkoa kwa kushirikiana na Wakurugenzi wa Halamshuri za Wilaya Mkoani Dodoma kuratibu kwa ufanisi masuala ya ikama ya walimu na usambazaji wa walimu kwa kuangalia mahitaji halisi ya kila eneo kwenye Mkoa na kupeleka Walimu kwa mgawanyo unaozingatia mahitaji, na kuepusha kupanga walimu wengi eneo moja wakati maeneo mengine yanakosa walimu. Aidha, kikao kilishauri TAMISEMI kuacha utaratibu wa kuwapanga walimu moja kwa moja kwenye wilaya au vituo husika badala yake kazi hiyo iachiwe Mkoa na Halmashauri za Wilaya.

•Kamati iliagiza Halmashauri zote za Wilaya Mkoani Dodoma kwenda kujipanga na kujenga miundombinu na kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza kwa Mwezi Januari mwaka 2018 wanakwenda kidato cha kwanza pasipo kubaki hata mwananfunzi mmoja.

•Viongozi watoke maofisini wafanye ziara za kukagua shule kujionea hali halisi na changamoto za elimu

Kuboresha Usimamizi wa Kilimo na Kuondoa tatizo la Upungufu wa Chakula katika Mkoa

•Kamati ilielekeza Wilaya kujipanga kuimarisha zao la Korosho kama zao la biashara lililoonekana kuwa na uwezo wa kufanya vizuri kwenye Mkoa wa Dodoma

•Ilielezwa kuwa tafiti za wataalamu wa kituo cha Naliendele zimethibitisha Ardhi ya Mkoa wa Dodoma na hali yake ya hewa vina uwezo mkubwa wa kustawisha na kuzalisha Zao la Korosho, Wilaya zimeagizwa kuanzisha na kusimamia kilimo cha zao la korosho kwa kuhakikisha matumizi ya mbegu bora za kisasa za korosho kutoka Kituo cha Naliendele Mtwara (Mbegu tani 9.1/Mkoa wa Dodoma) kwa kuotesha miche na kuisambaza kwa wakulima. (Baadhi ya Wilaya zimeshaanza - Mpwapwa)

•Kamati iliagiza viongozi na wataalamu wa kilimo kwenda kuwasimamia wakulima wazalishe mazao yanayostahimili na kutumia maji kidogo kulingana na hali ya hewa ya Mkoa wa Dodoma na upatikanaji wake wa mvua, mazao kama mtama, uwele, mihogo, alizeti n.k ili kuondoa tatizo la upungufu wa chakula kwenye Mkoa wa Dodoma.

•Kamati iliagiza Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma kuwa na Daftari la Kilimo na kuanza utaratibu wa kulitumia ipasavyo, Daftari hili litatoa maelekezo yote muhimu ya kilimo bora kwa Mkoa wa Dodoma, taarifa za wakulima, maafisa ugani na taarifa za ukaguzi na usimamizi wa kilimo.

•Aidha, kamati iliwataka maafisa ugani kutekeleza kazi zao ipasavyo na kitaalamu tofauti na ilivyo sasa maafisa ugani hawatekelezi majukumu yao kwa ufanisi.

•Katika minada ya mazao na mifugo, Kamati ilielekeza Halmashauri za Wilaya kuhakikisha kuwa minada yote inakuwa na huduma muhimu za Maji ya uhakika, Huduma za Vyoo na kuboresha maeneo/miundombinu ya kuchinjia mifugo

•Kamati ilipitishwa na kuubariki “Mpango wa kupunguza Umaskini na Kuongeza Usalama wa Chakula kwenye Mkoa wa Dodoma” ambapo Wilaya zilitakiwa kwenda kuanza kuusimamia. Mpango unazitaka kila Wilaya ya mkoa wa Dodoma kuchagua vijiji vitatu (3) vya kuvisimamia na kila kijiji kuteuwa kaya tano (5) maskini za kuzisimamia kwenye kilimo kama sehemu ya mfano kwenye kulima mazao yanayoshauriwa hapa Dodoma; Aidha; mpango unaelekeza pia kufuga kuku

Afya na Usafi wa Mazingira

•Kamati ilipitishwa na kujadili mpango wa ujenzi wa wodi mpya kutoka msaada wa fedha zilizotolewa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli (100 Mil.) na Kampeni ya usafi wa Mazingira.

•Mkoa umeonelea fedha hizo Mil 100 kutoka kwa Mheshimiwa Rais zitatumika kujenga Wodi ya Mifupa kwa sababu mahitaji yake yanakuwa siku hadi siku hapa Makao Makuu ya Nchi.

•Kwa sababu ya ufinyu wa Eneo la Ardhi, Mkoa umeonelea utajenga ghorofa mbili ambapo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma itaongeza kiasi cha Shilingi 100 Mil. na kufanya jumla ya fedha zote kuwa Mil. 200.

•Hatua inayoendelea kwa sasa ni uchoraji wa ramani ili kujua mahitaji halisi ya mradi huo na gharama zake.

•Katika Usafi, Mkoa umeanza Kampeni ya kufanya Usafi wa Mazingira Jumamosi ya kila Wiki ili kuongeza Ari zaidi ya kufanya Usafi, kampeni hiyo inahusisha pia zoezi la ushindanishi wa kataa na mitaa katika kufanya usafi na kutangaza matokeo katika vyombo vya Habari.

•Aidha, Kamati iliagiza pia zoezi hili la kufanya usafi kila jumamosi ya kila wiki liende hadi wilayani, vijijini kwa kuwa hali na viashiria vya usafi haviridhishi na tayari kumekuwepo na magonjwa ya milipuko kwenye baadhi ya maeneo.

•Aidha, kampeni ya Usafi pia inaenda sambamba na Kampeni ya Kusikiliza kero mbalimbali za wananchi kwenye kata zao ambapo baada ya zoezi la usafi kumalizika inafuatiwa na awamu ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.

•Kamati iliagiza Mamlaka zinazohusika kuweka mkakati wa kudhibiti uchafuzi wa mazingira barabarani na maeneo yanayopakana unaofanywa na magari ya kusafirisha abiria na mizigo kama kutupa taka, plastic bags na uchimbaji dawa.

•Kamati iliziagiza Wilaya zote kuanza mara moja utekelezaji wa kampeni ya Upandaji miti iliyozinduliwa na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na kuwa zitumie mvua hizi za mwanzo kupandia miti.

•Aidha, Kamati iliziagiza Halmashauri za Wilaya kupanda miti pembezoni mwa barabara zinazoingia na kutoka Mkoani Dodoma ili kutengeneza ukanda za kijani (Green Belt)

Utekelezaji maelekezo ya Serikali ya Uanzishaji Viwanda

•Halmashauri za Wilaya zimeelekezwa kujitathimini na kujipanga namna ya kuvutia wawekezaji wa viwanda

•ili kuvutia wawekezaji wa viwanda, Halmashauri za Wilaya zimeelekezwa kuyaendeleza/kuyaboresha maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya viwanda kwa kuyawekea miundombinu yote muhimu kama barabara, umeme, maji n.k

Ukusanyaji Mapato na Bajeti

•Halmashauri za Wilaya zilielekezwa kuwa suala la kutumia mashine za kielectronic kukusanyia mapato siyo jambo la hiari ni la lazima, na pia litazisaidia Halmashauri za Wilaya kuongeza ukusanyaji mapato yake, Kila mwaka Halmashauri zitenge fedha kwenye Bajeti zake na kununua  mashine hizo za kielektroniki kulingana na mahitaji ya mashine hizo kwa kila Halmashauri.

•Kwa kuzingatia kuwa Serikali imeshahamia Dodoma Makao Makuu ya nchi yetu, Dodoma inahitaji kujipanga na kutekeleza miradi na shughuli mbalimbali za maendeleo ambazo zote hizo zinahitaji fedha ili kuwezesha utekelezaji wake; Kamati ilitoa wito kwa Serikali kutoa Fedha zote zilizoombwa na Mkoa katika bajeti yake na pia Serikali itoe Fedha hizo kwa wakati.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.