• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MAAFISA ELIMU WATAKIWA KUJIPAMBANUA KUONGEZA UFAULU NA UBORA WA ELIMU

Imetumwa : March 18th, 2025

Na. Francisca Mselemu

       Habari - Dodoma RS


Hayo yamebainishwa na  Katibu tawala Mkoa wa Dodoma, Ndugu Kaspar K. Mmuya Machi 18, 2025 wakati akifungua mafunzo ya Maafisa Elimu Kata, yalioandaliwa na Mradi wa Shule Bora chini ya ufadhili wa UK - Aid na kufanyika katika ukumbi wa Kondoa Irangi, Wilayani Kondoa.


Katibu Tawala amewaeleza Maafisa hao kuwa wao ndio wenye jukumu la kusimamia elimu katika kata zao, kwa kuzingatia hilo watimize majukumu yao, kwa kuwa wana dhima kubwa ya kuhakikisha Mkoa unafikisha 95% ya ufaulu kama yalivyo maelekezo ya Mkuu wa Mkoa ,Mheshimiwa Rosemary Senyamule.


"Dodoma ni Makao makuu ya Nchi, kila kinachofanyika kiendane na hadhi ya Makao Makuu.Tujipambanue kwa kuongeza ufaulu na ubora wa elimu".RAS Mmuya.


Katibu Tawala ametoa Rai kwa Maafisa hao kuishi kimkakati kwa kununua Ardhi- katika Jiji la Dodoma kwani  Ardhi inaongezeka thamani, hivyo itawasaidia watakapokuwa wamestaafu.


Kadhalika amewahimiza juu ya upendo,ambapo amesema kuwa muda wao mwingi wanautumia kazini hivyo ni vema wakawa na upendo na ushirikiano baina yao  ili waweze kuishi vizuri, lakini pia wasimamie maslahi ya walimu na wanafunzi katika kata zao ili walimu na wanafunzi hao wawe na furaha. Kwa kufanya hivyo ufundishaji na ujifunzaji utakuwa wenye matokeo.


Naye Katibu Tawala Msaidizi  Seksheni ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Mwalimu Vicent B. Kayombo amewaasa  Maafisa hao kufanya kazi zao kwa bidii , akisisitiza kuwa baada ya mafunzo hayo, wote waliokuwa hawafanyi kazi vizuri wakajirekebishe.


"Msimamo wangu, fanyeni mambo yote, kama una biashara fanya, kama unalima lima, fanya chochote kinachokuongezea kipato, lakini fanya kazi, usiache kufanya kazi inayokujengea heshima. Kazi ndio imekuwezesha kukopa ukaanzisha hiyo biashara, kwa nini usifanye kazi? Ni lazima mjifunze 'kubalance' mambo. Mwl. Kayombo.


Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa Shule Bora Mkoa wa Dodoma  Bw. Mtemi Zombie, amesema muelekeo wa Wafadhili  wa Mradi huo kwa sasa ni kuunga mkono  ubunifu wa kuongeza thamani kwenye majukumu yao, mambo ya kawaida kawaida sio muelekeo wao, hivyo amewahimiza Maafisa Elimu Kata kuwa wabunifu na wanapofanya ubunifu watangaze ubunifu wao kama umeleta tija kwa kufanya hivyo, wataonekana.



Ameongeza kuwa kutokana na kufanya vizuri kwa Mkoa huu, Wafadhili wameamua kuendelea na mradi, hivyo watamalizia maboma yote katika namna ileile ya kupunguza joto kama walivyofanya katika awamu ya kwanza ya ukamilishaji wa maboma ya madarasa ya mfano.


Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo  Afisa Elimu Kata kutoka Halmashauri ya Mji Kondoa, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Maafisa Elimu Eugen Shirima ,amewashukuru Shule Bora kwa mafunzo hayo, pia amewashukuru Viongozi kwa nasaha walizowapa, yeye

pamoja na wenzake wameyazingatia na watayafanyia kazi maelekezo yote.


Mafunzo hayo ya siku moja yenye lengo la kuwajengea uwezo  Maafisa hao, yamewakutanisha  Maafisa Elimu Kata, Wathibiti Ubora  wa Shule pamoja na Maafisa Elimu Msingi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma.




 #dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangu, birthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • KAMPUNI YA "CAVO'' YA CHINA YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

    May 05, 2025
  • TAWLA - SAUTI YA WANAWAKE NA WATOTO WALIOKOSA ULINZI WA KISHERIA KATIKA JAMII

    May 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.