• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MAPOKEZI YA KATIBU TAWALA MPYA WA MKOA WA DODOMA DKT. FATMA MGANGA: AAHIDI UTENDAJI ULIOTUKUKA, ATAKA MKOA WA DODOMA KUWA MSHINDI KWENYE NYANJA ZA MAENDELEO

Imetumwa : June 3rd, 2021

Katibu Tawala Mpya wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatma Mganga, leo Juni 3, 2021 amepokelewa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na kuanza rasmi majukumu yake huku akiahidi utumishi uliotukuka katika kuwahudumia wananchi na kutatua changamoto zinazoukabili Mkoa wa Dodoma kwenye Sekta za Elimu, Uchumi, Afya, Kilimo, Mifugo na huduma nyingine za jamii kwa ujumla.

Dkt. Mganga ameyasema hayo leo wakati wa hafla ya kumpokea iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Anthony Mtaka wakati alipowasili kwa mara ya kwanza kama Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Dodoma kufuatia kuteuliwe kwake hivi karibuni na kuapishwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan Juni 2, 2021 kushika wadhifa huo.

Dkt. Mganga amesema kuwa yeye ni muumini wa kuibuka mshindi kwenye sekta zote muhimu anazozisimamia na hivyo amewataka watumishi wote wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Halmashauri za Mkoa wa Dodoma na Taasisi zote katika Mkoa huo kuwa na nidhamu, bidii na ubunifu katika kazi.

“Natambua Mkoa wa Dodoma una kabiliwa na changamoto ya Elimu na kwa muda mrefu Mkoa umekuwa na matokeo yasiyoridhisha katika mitihani ya Taifa huku ukishika nafasi ya 20 kushuka chini” Alisema Dkt. Mganga huku akiongeza kuwa ni jukumu la wanadodoma wote kushirikiana na uongozi mpya wa Mkoa kuhakikisha hali hiyo inabadilika.

Akizigeukia Halmashauri za Mkoa wa Dodoma, Dkt. Mganga amesema kuwa anatambua changamoto zinazozikabili Halmashauri za Mkoa huo huku akiahidi kuzisimamia na kuzishughulikia akianzia na mgogoro unaoletwa na utofauti wa malipo ya waheshimiwa madiwani katika Halmashauri moja hadi nyingine za Mkoa wa Dodoma.

Aidha, ameahidi kuzisimamia kwa nguvu Halmashauri za Mkoa wa Dodoma kuhakikisha zinatenga asilimia 40% ya mapato yake na kupeleka kwenye miradi ya maendeleo na kupeleka asilimia 10% za mapato kwenye mikopo ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka akitoa salamu za kumkaribisha Dkt. Mganga alisema kuwa, ana imani kubwa nae na kuwa amekuwa na utendaji uliotukuka uliopelekea kupanda madaraja kutoka mtumishi wa kawaida, Mkuu wa Idara, Mkurugenzi wa Halmashauri na hadi sasa ni Katibu Tawala wa Mkoa.

“Dkt. Mganga amekuwa na rekodi nzuri ya kiutendaji wakati akiwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi na Halmashauri hiyo wakati wa kipindi chake imekuwa Halmashauri ya mfano katika Mkoa wa Dodoma na maeneo mengine ya nchi, hivyo natarajia atayaendeleza hayo yote akiwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma” aliongeza Mhe. Mtaka.

Akimuwakilisha Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma Meja Mstaafu Risasi Salingwa, amesema kuwa ili Mkoa uweze kufanikiwa na kupiga hatua lazima viongozi wa Mkoa wa Dodoma wawe na sifa za kukubali kushauri na kushauriwa, waelewe hali ya wakati uliopo na aina ya wananchi wanaowaongoza,  waongoze kwa mifano na matendo bora, watumie lugha thabiti ya kiungwana, wagawe madaraka kwa wasaidizi wao na kufuatilia mrejesho wa majukumu.

Aidha, waondoe ukabila, udini na makundi ya aina zote, wazuie migongano kwa kutumia njia ya vikao na majadiliano ya mikutano na wakumbuke kuwaendeleza watumishi kwa kuwapeleka masomoni, mafunzo, kutoa motisha ya kutambua utendaji wao na pia kuwapandisha vyeo na maslahi yao, alimalizia Mwenyekiti huyo.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • DODOMA YADHAMIRIA KUJIKITA KWENYE KILIMO CHA MATUFAHA (APPLES) KUINUA UCHUMI

    May 08, 2025
  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • KAMPUNI YA "CAVO'' YA CHINA YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

    May 05, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.