• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MGUSO WA KIPEKEE WA MHE.RAIS SEKTA YA AFYA,WAVUTA WADAU KITUPO CHA AFYA MKONZE

Imetumwa : March 11th, 2025

Na. Hellen M. Minja,

       Habari - DODOMA RS


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametajwa kuwa na mguso wa kipekee kwenye sekta ya Afya kwa kufanikisha huduma bora sambamba na uwepo wa vifaa tiba kwenye vituo vingi vya afya hapa Nchini, hali inayovutia wadau zikiwemo Taasisi Binafsi kuchangia upatikanaji wa huduma hiyo adhimu.


Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule Machi 11, 2025, alipoalikwa katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa na vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi Milioni tisa kutoka Benki ya Stanbic Mkoni hapa katika Kituo cha Afya cha Kata ya Mkonze Jijini Dodoma.


Akizungumza na Watumishi wa kituo hicho pamoja na wakazi wa eneo hilo ambao ndio wanufaika wa huduma zinazotolewa na kituo hicho, Mhe. Senyamule amesema;


"Ndugu zangu haya mambo sio madogo ni makubwa na tunayasema kwa sababu ni mapinduzi yaliyotokea katika kipindi kifupi kwa sababu ya dhamira ya dhati ya Kiongozi wetu Mkuu na mguso wake wa pekee kwa maendeleo ya wananchi wake lakini leo kwa maendeleo ya sekta ya Afya.


"Stanbic Benki wameona Mhe. Rais ameweka hapa chumba cha kujifungulia, Madaktari wa upasuaji na mashine za X- Ray. Wagonjwa wameongezeka, baadhi ya vifaa vimekua vichache kutokana na ongezeko hilo wakasema hapana, sisi kama Benki, Mhe. Rais ameshafanya vingi, tuchukue sehemu yetu tukaongeze nguvu kwenye kazi ya Mhe. Rais." RC Senyamule.


Aidha, Meneja wa  Benki ya Stanbic Dodoma Bi. Joan Mbise, ameainisha vifaa na vifaa tiba hivyo ambavyo ni mashuka, vyandarua, pazia za kutenganishia vitanda, vifaa vya upasuaji na miche 150 ya miti ya matunda akisema kuwa, huo ni ushahidi wa dhamira yao ya dhati kuendelea kusaidia maendeleo ya Jamii pamoja na utunzaji wa mazingira.


Vilevile, Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho cha Afya Halima Kheri, ametaja huduma zinazotolewa na kituo chake  kuwa ni huduma za Baba, Mama na Mtoto, upasuaji wa dharura, wagonjwa wa nje na ndani, kujifungua, meno, maabara, dawa, tiba na matunzo kwa wanaoishi na Virusi vya Ukimwi na Kifua Kikuu, mionzi na pia wameanzisha huduma ya kuhifadhi maiti.


Kituo cha Afya Mkonze ni miongoni mwa vituo 7 vya Halmashauri ya Jiji la Dodoma,kilianzishwa mwaka 1993. Kinahudumia wakazi 41256, Kaya 11006, mitaa 8 na Zahanati 9 zilizopo katika Tarafa ya Zuzu. Kituo kina Watumishi 59 wa Kada mbalimbali na kimehudumia wagonjwa 207,600 kwa mwaka 2024 ambao ni wastani wa wagonjwa 565 kwa siku.



 #dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • KAMPUNI YA "CAVO'' YA CHINA YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

    May 05, 2025
  • TAWLA - SAUTI YA WANAWAKE NA WATOTO WALIOKOSA ULINZI WA KISHERIA KATIKA JAMII

    May 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.