• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mhe. Mtaka Asikiliza Kero za Wana Mtera , Awataka Viongozi Kutoka Maofisini Kutatua Kero za Wananchi

Imetumwa : July 18th, 2022

 Ikiwa ni sehemu ya kusikiliza kero za wananchi wa Mkoa wa Dodoma, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka akiwa ameambatana na Katibu Tawala wa Mkoa pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama hivi karibuni wametembelea wananchi wa Mtera ili kusikiliza kero zao ambapo kero yao kubwa ni upatikanaji wa maji safi na salama.

Kabla ya kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Mtera Mhe. Mtaka pamoja na ujumbe wake wametembelea mradi wa bwawa la maji la Mtera pamoja na eneo ambalo tenki la maji litajengwa.

Akizungumzia mradi huu,meneja wa RUWASA wilaya ya Mpwapwa Eng,Warioba ameeleza kuwa mradi huo ulianza mwaka 2020, ni  mradi wenye thamani ya Tsh.1.7 Bln ambapo mpaka sasa wamepokea Tsh.700mln. Mradi huu  unajengwa kwa kutumia Force Akaunti, mradi huu unategemea kukamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi Julai,2022. Mara utakapokamilila  mradi huu utawanufaisha wanachi zaidi ya 1.036mln. Aidha Eng.Warioba ameeleza kuwa baadhi ya sababu zinazochelewesha  mradi huo ni pamoja na upatikanaji wa mabomba ya chuma na uchelewevu wa  upatikanaji wa fedha za mradi.

Mkuu wa Wilaya Mpwapwa Mhe. Maganga ameeleza kuwa pamoja na mradi huo wa maji wenye thamani ya Tsh. 1.7Bln kuanza miaka miwili iliyopita bado kuna changamoto nyingi ambazo zimekuwa zikileta kero kwa wananchi. Changamoto hizo ni pamoja na kutokuwepo kwa nyaraka za ukusanyaji wa mapato , kutokuwepo kwa nyaraka zinazoonyesha idadi ya watuaji wa maji baadhi ya miundo mbinu haijakamilika, utekelezaji wa kurekebisha koki na mivujo haifanyiki kwa wakati na hivyo kusababisha upotevu wa maji. Vitu ambavyo havijakamilika mpaka sasa kwenye mradi huu ni chujio la maji, ofisi na  sehemu ya kunyweshea Mifugo,aidha maji yanayopatikana hapa yana chumvi mno. Aidha Mkuu wa Wilaya huyo amewataka wananchi wa mtera kueleza matatizo yao kwa ukweli na uwazi kwani lengo la kikao cha  Mkuu wa Mkoa pamoja nao ni kusikiliza kero za wananchi wa Mtera.

Baada ya maelezo hayo ya utangulizi ,Mkuu wa mkoa ametoa fursa kwa wananchi kueleza kero zao ambapo nyingi ya kero hizo zilijikita katika kutoridhishwa na utekelezaji wa mradi wa maji, ukosefu wa maji safi na salama,kutokushirikishwa, viongozi kutokuwajibika ipasavyo,TASAF- kutofika kwa walengwa, shule ya bweni ilijengwa na mfadhili kutokutumika, huduma ya kituo cha afya haipo vizuri kwani hakuna dawa, ukosefu wa huduma za kifedha, hela za SACCOS yao zililiwa.

Akijibu baadhi ya kero hizo Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatuma Mganga ameeleza kuwa suala la ushirikishwaji ni la kiongozi wa kijiji kwani kiongozi wa kijiji ndio anatakiwa kushirikisha  wananchi na kisha aite wataalam na katika mkutano wa wananchi. Si kazi ya mtaalam kushirikisha wananchi bali ni kazi ya mtendaji na mwenyekiti.

Akizungumzia Miradi inayoendeshwa kwa kutumia Fosi akaunti, Dkt. Mganga amesema mradi wotewote unaotumia force akaunti  ni lazima uwe na kamati tatu, kamati ya ujenzi, Kamati ya manunuzi na kamati ya  mapokezi. Kamati zote tatu  zinatakiwa ziundwe na zisimamie vyema mradi. Watu wafanye kazi bila majungu.Safari ijayo nataka tupate taarifa toka kwa kamati na sio wataalam.

Aidha Dkt. Mganga aliwakumbusha viongozi kuwa Kiongozi hupaswi kualikwa kwenye mradi, badala yake kiongozi unatakiwa  kuwa na kimbelembele. Kila kiongozi asimamie mradi kwa nafasi yake yote. Ni lazima  muwe na ratiba ya kufuatilia miradi na kutembelea miradi. Kila mnapofanya vikao vyenu hakikisheni mnatembelea mradi  angalau mmoja na kuangalia maendeleo yake.Mnapaswa kuorodhesha mradi yote ambayo haijakamilika ili Tamisemi watume fedha na hayo maboma yakamilike. Asilimia 40 inatakiwa itumike kumalizia miradi viporo ili kutekeleza kazi

Kuhusu suala la SACCOS, ni vyema  afisa ushirika aje kufanya upembuzi yakinifu  wa mkoa, na waliokula fedha sheria ichukue mkondo wake. Kuhusu TASAF- nipende kuwaambia kuwa, kuwa kwenye TASAF sio sifa, wanaongia kwenye TASAF ni maskini. Ni vyema hiyo nguvu unayotumia kudai TASAF ukaitumia kuzalisha hasa wakati unaguvu zako. Cha msingi tuanze kujiwekea akiba toka ujanani. Tutahakikisha TASAF wanapata wale ambao ni maskini kweli. Cha Muhimu unapokuwa na nguvu za kuzalisha basi tuzalishe. 

Kuna majukumu ya Serikali na majukumu ya mtu mmoja mmoja hivyo ni muhimu kila mmoja akafanya jukumu lake.Kuhusu huduma ya kituo cha afya nitaongea na  Mganga Mkuu Mkoa ili kuhakikisha vifaa vinaletwa mara moja.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka amewaagiza viongozi kutoka maofisini na kutatua kero za wananchi, badala ya kukaa ofisini  mkisubiri ziara ndio mtembelee miradi ni jukumu lenu kutoka maofisini kutembelea miradi na kutatua kero za wananchi."Haingii akilini mradi umeanza 2020 lakini hadi leo hii viongozi humjatembelea mradi halafu bado unafanya kikao kujadili mradi ambao hata hujui ukoje” amesema Mhe. Mtaka.

Suala la kuandaa maisha ni suala la Muhimu sana.Tuimarishe elimu ya sekondari ya kata  Idara ya Elimu kaeni  vizuri na Wanafunzi na muangalie namna njema ya kuongeza ufaulu.Tunzeni ardhi, haya Haya maji na udongo ni mali. 

'Ninawapa siku 65 tarehe 25/9/2022 tutakuja tena kijiji cha Mtera kufanya kikao na wananchi na kuwakabidhi mradi wa maji safi na salama" Ameagiza Mhe. Mtaka.

Aidha Mhe. Mtaka ametumia fursa hiyo  kuwakumbusha wananchi wa Mtera mambo ya msingi matatu ambayo ni Sensa ya watu na makazi 23/8/2022,Sherehe za 88 Nzuguni Dodoma 30/7-10/8/2022, wenye bidhaa za kuonyesha wenye bidhaa za kununua, ufugaji, kilimo  wote waje kuonyesha bidhaa zao pamoja.Vilevile Mkuu wa Mkoa amewakumbusha wananchi w mtera kuwa 25/7/2022  itakuwa  Sherehe za mashujaa ambayo itafayika katika viwanja vya mashujaa  na mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais. Samia Suluhu Hassan.

 MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’ YAIVA

    May 08, 2025
  • DODOMA YADHAMIRIA KUJIKITA KWENYE KILIMO CHA MATUFAHA (APPLES) KUINUA UCHUMI

    May 08, 2025
  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.