• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MHE. SENYAMULE AONGOZA UPANDAJI MITI MZAKWE

Imetumwa : January 2nd, 2023

MITI 5,300 YAPANDWA BONDE LA MZAKWE

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameongoza zoezi la upandaji miti katika eneo la chanzo cha maji cha bonde la Mzakwe zoezi ambalo ni muendelezo wa kampeni ya upandaji miti ngazi ya Mkoa iliyozinduliwa rasmi Desemba 31 kwa kupanda miti kwenye eneo la chanzo cha maji cha DUWASA kilichopo eneo la Ihumwa vijijini.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo Mhe. Senyamule amewataka  wasimamizi wa Bonde la Wawi-Ruvu, wadau wa mazingira na wananchi kulipa  bonde hilo usimamizi madhubutu bila kusukumwa kwani kila mmoja anapaswa kutambua wajibu wake juu ya kulilinda eneo hilo la hifadhi kutokana na umuhimu wake

“Tuna imani kuwa utafiti wa kutosha ulikwishafanyika hapa hivyo tutaona miti itakayopandwa ikikua kwani hauwezi kupanda miti eneo ambalo halijafanyiwa utafiti wowote ni matumaini yangu kuwa kama utafiti  ulifanyika kweli, basi tutaona miti ikikua vizuri na sio kufa” Amesema Mhe. Senyamule

Ametoa msisitizo kwa wasimamizi wa eneo hilo kuhakikisha wanalitunza eneo la bonde la Mzakwe ili kupoteza historia mbaya iliyowahi kutokea miaka ya nyuma ya miti kutoota katika eneo hilo, miti kuungua moto na uvamizi wa wananchi kwa kuweka makazi katika vyanzo vya maji na kusababisha uharibifu wa mazingira.

“Tuna imani kubwa miti hii mtaitunza, itakua na kupoteza historia yote ambayo ilitokea katika bonde hili la Mzakwe. Ni wajibu wetu kutunza vyanzo vya maji kwa ajili ya matumizi ya maeneo mbalimbali. Sitatamani kuona uzembe wowote ambao utatokea wa kufanya miti hii isikue, nitoe onyo kwa wananchi ambao ni chanzo cha uharibifu wa miti hii kwa kuchoma moto na  kuleta mifugo kwenye hifadhi kuwa ni kinyume cha kisheria na tutawachukulia hatua” Ameongeza Mhe. Senyamule.

Naye Bi. Feliciana Mpanda ambaye ni Afisa Kidaki cha Maji Wami-Ruvu, amesema chanzo hiki ni muhimu kwakuwa kinategemewa kuzalisha maji takribani lita Milioni131 yatakayotumiwa na Jiji la Dodoma licha ya changamoto zinazolikabili bonde hili. Amezitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na uingizaji wa mifugo na uchomaji moto unaofanywa na wananchi wanaozunguka bonde hilo na kutoa rai kwa jamii ukabililiana na changamoto hizi ili kulilinda bonde.

Vilevile, Afisa wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Bw. Frank Chombo, ameainisha aina 4 ya miti inatakayopandwa katika eneo hilo kulingana na tafiti za udongo zilizofanyika kwenye eneo hili na kuhimiza wananchi kufika kwenye bustani za Wakala wa Misitu Tanzania kote nchini kuchukua miche kwakuwa inapatikana kwa wingi. Kwa wakazi wa Dodoma, amesema bustani zipo maili mbili na eneo la Ikowa katika Wilaya ya Chamwino, pia wana miche zaidi ya Million 1 inayo gawiwa bure.

 

Takriban miti 5,300 imepandwa katika bonde la Mzakwe katika kipindi cha mwezi mmoja na kampeni hii ni endelevu na lengo ni kupanda miti 40,000 ndani ya miaka minne.

 

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.