• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MKOA WA DODOMA WAENDELEA NA UTEKELAZAJI WA MPANGO WA KIFUA KIKUU

Imetumwa : January 31st, 2025

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS

Kufuatia changamoto ya uibuaji Wagonjwa wa Kifua  Kikuu kuelekea kwenye lengo la Dunia la kutokomeza ugonjwa huo ifikapo 2030, Seksheni ya Afya Mkoa wa Dodoma chini ya Wizara ya Afya, leo Januari 31, 2025, wamefanya kikao kazi cha kujadili namna ya kufikia lengo la uibuaji wagonjwa kwa kushirikiana na vituo binafsi vya afya na Wadau.

Akizungumza na wadau hao katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma jengo la Mkapa Jijini Dodoma, Mganga Mkuu wa Mkoa Dr. Thomas Rutachunzibwa, ameelezea umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali na vituo binafsi ili kufikia malengo lakini pia ametoa angalizo juu ya utoaji ‘takwimu hewa’ za wagonjwa wa Kifua Kikuu.

“Niombe wenzetu wa vituo binafsi, tusaidiane kuwahudumia wananchi tuhakikishe kwamba lengo tulilopewa tunalifikia ikiwezekana na kulizidisha sio tunafikia hilo lengo na kusema tumemaliza, haya malengo ni makisio tu, kama umepewa wagonjwa 10 lakini uhalisia kuna wagonjwa 20, waibue wote.

“Tusije tukaleta takwimu hewa, ukisema nimeibua 10 kumbe humo kuna watatu ambao sio wagonjwa, tutakwenda kuaibika huko mbele. Naomba turipoti wagonjwa wa kweli na tujitahidi kadri tunavyoibua kwa siku, takwimu zinaingizwa kwenye mfumo. Baadhi ya Halmashauri wamekua wakifanya kazi nzuri lakini ukija kwenye mfumo, hakuna taarifa,” Dr. Rutachunzibwa.

Akielezea malengo ya Mpango huo, Mratibu wa Huduma za kudhibiti Kifua Kikuu kutoka Wizara ya Afya Dkt. Allan Tarimo, amesema Mpango huo una malengo makubwa matatu ambayo ni kupunguza vifo kwa 75% ikilinganishwa na mwaka 2015, kupunguza maambukizi kwa 50% na kupunguza changamoto za kiuchumi kwa mgojwa kwa 50%.

Kadhalika, Mratibu wa Kifua Kikuu na ukoma Mkoa wa Dodoma Dkt. Peres lukango amesema, huduma za Kifua Kikuu zimejengwa kwenye utashi binafsi, hali inayosababisha huduma kushuka pindi Mtaalamu anapoondoka kwenye kituo husika hivyo, inapaswa huduma hizo ziwe sehemu ya kituo kizima na si mtu binafsi ili kufikia malengo.

Hata hivyo, Mwakilishi kutoka Hospitali ya Mt. Gemma ya Jijini Dodoma ambayo ni moja ya vituo vinavyotoa huduma za Kifua kikuu Dkt. Theodora, amesema Hospitali yake imepewa lengo la kufikia wagonjwa 16 na mpaka sasa wameshafikia wagonjwa 11 hivyo wanatarajia kufikia malengo waliyowekewa na zaidi.

Mkoa wa Dodoma ni miongoni mwa Mikoa 9 iliyo kwenye Mpango Harakishi wa kuibua wagonjwa wenye vimelea vya Kifua Kikuu Mpango ambao ulizinduliwa rasmi Januari 06, 2025 katika Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma na Waziri mwenye dhamana ya Afya Mhe. Jenista Mhagama.


#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • KAMPUNI YA "CAVO'' YA CHINA YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

    May 05, 2025
  • TAWLA - SAUTI YA WANAWAKE NA WATOTO WALIOKOSA ULINZI WA KISHERIA KATIKA JAMII

    May 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.