• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MRADI WA BARABARA YA MACHINGA WAKABIDHIWA KWA MKANDARASI

Imetumwa : October 31st, 2023



Mradi wa ujenzi wa barabara ya Machinga complex yenye urefu wa Km 0.65 kwa kiwango cha lami, umekabidhiwa kwa mkandarasi Oktoba 30, 2023. Hafla hiyo ya makabidhiano imehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule akiwa ndiye mgeni rasmi kwenye viwanja vya soko la Machinga Jijini Dodoma.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara hiyo, Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Dodoma Injinia Edward Lemelo, ametoa ufafanuzi wa namna utekelezaji wa Mradi huo utakavyofanyika.

"Ujenzi wa Machinga complex umesainiwa tarehe 25 Oktoba kwa shilingi 1,034,876,565.55 na Mkandarasi Nyanza Road Works Limited wa Dodoma kwa kipindi cha siku 180. Leo hii tupo hapa kwa ajili ya kumkabidhi eneo la mradi tayari kwa kuanza kazi. Kukamilika kwa matengenezo haya, kutarahisisha uingizwaji wa bidhaa sokoni na pia kutaboresha mazingira ya soko letu. Ujenzi huu utaambatana na ujenzi wa kitako cha barabara Km 0.65, matabaka manne ya barabara yaani G7, G15, C1 na CRR, uwekezaji tabaka la juu kwa lami ngumu yaani Asphalt Concrete Km 0.65, mitaro ya maji ya mvua Mita 1300 pande zote za barabara, uwekaji wa taa 20 za barabarani na njia za watembea kwa miguu" Amesema Injinia Lemelo.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule, amesema kuwa makabidhiano ya barabara hii kwa mkandarasi ni mwendelezo wa utekelezaji wa ahadi za ujenzi wa soko la Machinga zilizotolewa mwaka 2022 na amewausia kutunza mazingira ya eneo hili ili miradi idumu.

"Leo ni mwendelezo wa ahadi za Serikali kwenye soko hili, ikiwemo lami, uwekaji taa za barabarani na njia ya watembea kwa miguu zinawekwa kwa pamoja hivyo mkandarasi hakikisha unaharakisha ujenzi wa barabara hii uweze kukamilika nyuma ya wakati ili machinga waweze kufanya kazi zao saa 24. Pia natoka Wito kwenu mupande miti kwenye eneo hili kwani ni la wazi na litawezesha utunzaji wa mazingira kwani eneo hili linatembelewa na watu wengi kwa lengo la kujifunza kupitia mradi huu hivyo uzuri wa miundombinu hii utadumu endapo itatunzwa vizuri kwa kufanyika usafi" Mhe. Senyamule.

Vilevile, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe Jabir Shekimweri, ametoa rai kwa wananchi na Taasisi zinazohusika na upitishaji wa miundombinu yake kushirikiana na Mkandarasi kufanya tathmini ya njia za miundombinu yao ili kuzuia uharibifu pindi mradi unapokamilika. Pia amewataka wananchi kushirikiana na Mkandarasi wakati wa utekelezaji wa Mradi na wakati wa maudhi madogo madogo yatakayosababishwa na utekelezaji wa Mradi yatakapojitokeza.

Utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa barabara ya Machinga complex kwa kiwango cha lami unatekelezwa na Mkandarasi ajulikanaye kama Nyanza Road Works Limited chini ya Mhandisi Msimamizi ambaye ni Meneja wa TARURA Wilaya ya Dodoma. Mradi huu unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 6 (siku 180)
ent from my iPhone

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MMUYA AHIMIZA UDHIBITI VIFO VYA MAMA NA MTOTO

    May 26, 2025
  • UHAKIKI ANUANI ZA MAKAZI KUANZA MEI 28 DODOMA

    May 26, 2025
  • WAWEKEZAJI WA VIWANDA KUTOKA DUBAI WABISHA HODI DODOMA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI KUTOKA TUME YA MADINI WAMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.