• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

NSSF KUFANYA UWEKEZAJI WA ZAIDI YA BILIONI 148 DODOMA

Imetumwa : December 20th, 2024

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), unatarajia kuanzisha uwekezaji ndani ya Makao makuu ya Nchi (Mkoa wa Dodoma) kwa kujenga jengo  la ghorofa 16 ,jengo ambalo gharama yake inakadiriwa kuwa zaidi ya shilingi za Kitanzania  Bilioni 148 likijumuisha hoteli yenye hadhi ya nyota tano.

Hayo yameelezwa leo Disemba 20, 2024 wakati wa hafla ya upandaji miti kwenye eneo lao la  uwekezaji lililopo Njedegwa Jijini Dodoma ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alikua mgeni rasmi.

“Hoteli hii itafungua fursa mpya ya kufanyika mikutano ya Kimataifa hapa Dodoma hivyo kuongeza mnyororo wa thamani pia itachangia kukuza utalii na kuzalisha ajira zaidi pamoja na kupendezesha Jiji letu la Dodoma. Niwapongeze kwa kuunga mkono juhudi za utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti leo hata kabla hamujaanza mradi”. Amesema Mhe. Senyamule.

Kadhalika, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bw. Masha Mshomba, amesema suala la uwekezaji ni jukumu la kipekee na linatakiwa kufanyika kwa umakini mkubwa ili kuleta kipato cha kutosha kwa kuwa fedha hizo ni za wananchi.

Akielezea namna mradi utakavyotekelezwa, Meneja Usimamizi wa Mradi NSSF, Mhandisi Helmes Pantaleo amesema;

“Mradi unatarajiwa kuwa na jengo la ghorofa 16 na umegawanyika katika sehemu tatu, kuna eneo la ofisi, hoteli na mall, eneo hilo   lina ukubwa wa zaidi ya mita za mraba 20,000, na eneo zima la uwekezaji lina ukubwa wa hekta 2.1, hoteli itakua na vyumba 20 pamoja na migahawa, maduka na ofisi za watu wa hoteli”

 Mradi huo unaotarajiwa kutumia miaka mitatu (2025 - 2028 ) hadi kukamilika kwake,utaanza  kutekelezwa mwezi Mei 2025, vibali vya ujenzi vimeshapatikana kutoka Benki Kuu ya Tanzania, Ofisi ya Waziri Mkuu, Msajili wa majengo na Wizara ya Fedha, hivvyo kufikia Aprili 2O25 maandalizi yote yatakuwa yamekamika.





#dodomafahariyawatanzania                              

#keroyakowajibuwangu #mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.