• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Yaja na Muarobaini wa Changamoto ya Mtaji

Imetumwa : July 11th, 2022

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma imekuja na muarobaini wa kutatua Changamoto ya Mitaji  kwa mwananchi mmoja mmoja  mara baada ya kupokea maombi ya mara kwa mara ya misaada kutoka kwa wananchi hao.Akizungumza jinsi ya kukabiliana na changamoto hiyo kwa wananchi wa Dodoma. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka, leo ametoa Mkopo wenye thamani ya Tsh. 13,642,800/- (Tsh. Milioni Kumi na tatu laki sita elfu arobaini na mbili na mia nane tu) kwa wananchi 16 wa Mkoa wa Dodoma.

Akizungumzia Upatikanaji wao Mhe. Mtaka ameeleza kuwa, hawa wananchi 16 ambao leo hii wanapokea mkopo kwenye akaunti zao za benki, ni wale ambao wmekuwa wakija mara kwa mara ofisini kwangu kuomba msaada Kwa Mkuu wa Mkoa.Hivyo nikaona hawa wananchi badala ya kuwapa mara Tsh. 5000/- au Tsh.10,000/- ni vyema  kuwafundisha kuvua ili waendelee kujitegemea badala ya kuwapa Samaki.Hivyo kila aliyekuwa anakuja kuomba msaada nilikuwa namuuliza anataka afanye nini ilia pate kipato? Na hatimae kumuagiza kila mmoja wao aandike andiko la anafikiria mradi gani na ataufanyaje huo mradi.

Hivyo fedha ambazo watapokea leo zimetokana na mawazo yao na maandiko yao. Katika kundi hili la watu 16 tuna wanafunzi wa kike na kiume ambao ni wahitimu wa vyuo vikuu lakini wamekosa ajira na kuamua kujiajiri, tuna kundi la watu wazima ambao wanalea wajukuu zao bila msaada wowote, tuna walemavu sababu ya aksident na ambao hawawezi tena kufanya kazi walizokuwa wanafanya awali.

Akizungumzia chanzo cha fedha hizo, Mhe. Mtaka ameeleza kuwa kwa kawaida kila  mwaka , Serikali huwa inatoa kwa  kila Mkuu wa Mkoa kiasi cha Tsh.20 mln (Political Vote) na wakuu wa Wilaya hupewa Tsh.5.0 mln.Fedha hizi zinapaswa zitumike kumsaidia  Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya katika mambo ya kijamii wakati anafanya ziara zake katika eneo husika.

Hivyo kutokana na changamoto ambazo hutokana na fedha za halmashauri kugawiwa kwenye vikundi ambapo wakati mwingine imekuwa vigumu kupata watu wenye maono yanayolingana, au kuchukua fedha kama kikundi na kisha kugawana kila mmoja na hatimaye kwa yule ambaye hafanyi vizuri kuwatia hasara.

 Kwa kuangalia nchi zingine zinavyofanya  kusaidia jamii kutokana na kuandika  andiko la pendekezo la biashara ( Call for Proposal), Ofisi ya Mkuu wa MKoa imeamua kuja na wazo la kuwasaidia wananchi wa Dodoma kwa kuwapa mikopo wananchi  mmoja mmoja kulingana na andiko lake. Mkopeshwaji atalipa Mkopo huo kwa kipindi cha miezi 10 Kwa riba ya 2%, Mkopaji  hahitaji kuwa na kikundi ili kunufaika na mkopo huo.

Kwa mwaka  huu tunaanza na Tsh 13.0 mln mwakani tutaongeza ifikie Tsh. 20mln. Nimeongea na mabenki na kuwashauri  kwenye pesa ya CSR kwa nini wasitoe kiasi fulani ili kuwasaidia watu wenye mahitaji badala ya kutoa mabati, mifuko ya Sementi na Matofali. Mategemeo yetu kwamba Kwa mwaka ujao wa fedha, Mkoa utatoa Tsh.20ml, hivyo hivyo Wakuu wa Wilaya pia naweza kufanya hivyo kwenye Halmashauri zao.

Mhe. Mtaka amewaasa wananchi hao kuwa “ kila unapofanya biashara pesa  unayopata unatakiwa uiweke kwenye akaunti yako ya benki, ili mtu wa Benki aweze kuona fedha zinavyopita.Tayari mmepewa mafunzo ya biashara, na utunzaji wa fedha. Mtarajio yetu ni kwamba baada ya  muda  watu watasimama kama wafanya biashara na wanafunzi hawasitishwa masomo yao, na atakayefanya vizuri atapewa mara mbili ya kiasi alichopokea sasa.Hivyo ni vyema  kila mmoja aheshimu mwanzo wa mwenzake.Hata miradi itakayokufa tutaangalia sababu ya hiyo miradi kufa”. Amesisitiza Mhe. Mtaka.

Aidha Mhe. Mtaka alitoa fursa kwa wananchi hao kueleza changamoto zao ambapo kila mmoja alieleza changamoto yake ambayo ilipelekea kuandika andiko la biashara. Wananchi hao wamepata mikopo kuanzia Tsh. 350,000/- hadi Tsh. 1,800,000/-  ambazo wameahidi kufanya ujasiliamali.

MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2020 January 15, 2021
  • MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2020 January 15, 2021
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021 SHULE ZA BWENI (WASICHANA NA WANAUME) . December 20, 2020
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA YA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2020 January 15, 2021
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KATIBU TAWALA SINGIDA AKABIDHI OFISI KWA KATIBU TAWALA DODOMA

    March 23, 2023
  • MACHINGA DODOMA WAMPONGEZA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

    March 23, 2023
  • KIWANDA CHA AINA YAKE KUJENGWA KONGWA

    March 17, 2023
  • WAFANYAKAZI WAASWA MSHIKAMANO MAHALA PA KAZI

    March 15, 2023
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Mkoa akiongoza siku ya maombi jijini Dodoma
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.