• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RAIS MAGUFULI AMWAGA PIKIPIKI MPYA KWA MAAFISA TARAFA WOTE MKOANI DODOMA, RC MAHENGE AWAONYA MAAFISA TARAFA KUTOZITUMIA PIKIPIKI HIZO KAMA BODABODA

Imetumwa : March 21st, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ametoa pikipiki 448 kwa maafisa Tarafa wote hapa nchini ambapo, Mkoa wa Dodoma wenye tarafa 28 umepata mgao wa pikipiki 28 kwa ajili ya Maafisa Tarafa wote wa Mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge, akikabidhi pikipiki hizo kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Patrobas Katambi kwa niaba ya Wakuu wa Wilaya wote wa Mkoa wa Dodoma ili wazikabidhi kwa Maafisa Tarafa Mkoani humo, amewatahadharisha Maafisa Tarafa wote Mkoani Dodoma watakaopewa pikipiki hizo, kutothubutu kuzitumia pikipiki hizo kwa kuzifanyia biashara ya Bodaboda.

Dkt. Mahenge amemuagiza Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma Gilles Muroto, kuwaelekeza Wakuu wa Polisi wa Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma, kuhakikisha wanawakamata na kuwachukulia hatua za kisheria Maafisa Tarafa wote watakao zitumia pikipiki hizo za Serikali kwa kufanyia biashara binafsi kama bodaboda badala ya kuzitumia kuwafikia wananchi kwenye maeneo yote ya Tarafa zao kusimamia utoaji huduma za kijamii, kiuchumi na kiutawala.

“Maelekezo yangu kwenu, hizi ni pikipiki za kazi za Serikali, sio pikipiki za bodaboda, matokeo yake, tunatarajia kuona Maafisa Tarafa mnafika kwenye maeneo yenu yote na kuwa mnawasilisha taarifa ya kazi mbalimbali kwenye maeneo yenu” aliongeza Dkt. Mahenge.

Alitumia hafla hiyo kumshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuwa, katika kipindi cha uongozi wake amefanya mengi kwenye sekta za Afya, Miundombinu ya barabara, viwanja vya ndege na sekta ya anga, usafiri wa majini, nishati, madini, elimu, ukusanyaji mapato na sasa katika kuboresha utendaji wa serikali, ameimarisha utendaji wa Maafisa Tarafa ambao ni kiungo muhimu kwa kuwawezesha usafiri wa pikipiki.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Maduka Kessy amesema Mkoa wa Dodoma una jumla ya Tarafa 28 na Mhe. Rais Magufuli amewapatia pikipiki Maafisa Tarafa wote wa Mkoa wa huo na kuwa jambo hili linaimarisha uwezo wa Maafisa Tarafa kuwafikia wananchi wote kwenye maeneo yao ya Tarafa na pia ufanisi katika kusimamia shughuli za serikali.

Akipokea Pikipiki hizo kwa niaba ya Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dodoma, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Patrobas Katambi amesema kuwa changamoto kubwa iliyokuwa inawakabili Maafisa Tarafa katika kusimamia na kutekeleza shughuli za Serikali kwenye ngazi za Tarafa ilikuwa ni ukosefu wa Usafiri na sasa Rais Magufuli ametatua changamoto hiyo kwa nchi nzima. Aidha, amewataka Maafisa Tarafa kwenda kuzitunza pikipiki hizo.

Akishukuru kwa niaba ya Maafisa Tarafa wote Mkoani Dodoma, Lucas Mbise Afisa Tarafa ya Zuzu Jijini Dodoma, amesema pikipiki hizo ni ahadi ya Mhe. Rais Magufuli aliyoitoa Juni 4, 2019 alipokutana na Maafisa Tarafa hao Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuahidi kuwapatia pikipiki kutokana na mazingira ya maeneo yao ya kazi ili kuwaongezea ufanisi.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.