• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RAIS SAMIA ATOA SULUHU MGOGORO WA ARDHI KINGALE - KONDOA

Imetumwa : February 4th, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa Suluhu kwenye mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya Miongo mitatu dhidi ya eneo lenye ukubwa wa ekari 7,495.74 lililopo kati ya Vijiji vya Kata ya Kingale katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na Gereza la King'ang'a ambalo ni eneo lenye rutuba kwa shughuli za kijamii za uzalishaji.

Suluhu hiyo imewasilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule kwa niaba ya Mhe. Rais na ameitoa mbele ya wananchi wa Kata hiyo wakiwa na viongozi wao.

"Ardhi yote ni mali ya Serikali, Waziri alipokuja hapa alifikisha hili jambo kwa Mhe Rais aamue na ametoa suluhu kwa Wanakingale. Amesema eneo lenye mgogoro la ukubwa wa ekari 7,495.74, ekari 3,272.4 zibaki kwa wananchi watumie kwa shughuli za kilimo, mifugo na za kiuchumi na Magereza watachukua ekari zilizobaki" amesema Mhe. Senyamule

Mbali na kuwasilisha utatuzi pia Mhe Rais ameagiza mambo kadhaa yafanyike katika eneo hilo;

"Mhe. Rais ameagiza kuwa ndani ya mwezi mmoja, watu wa ardhi waje kuonyesha utaratibu wa maeneo yaliyogawanywa, lipimwe na alama ziwekwe zinazoonekana na kila mmoja. Vijiji viendelee kutunza mipaka kuzuia mwingiliano wa matumizi, Magereza pia mtunze mipaka, wananchi wapo upande wa Bonde linalofaa kwa umwagiliaji. Wizara ya Kilimo mfanye utaratibu wa kujenda mabwawa kwa ajili ya umwagiliaji, mifugo pia mjenge majosho kwa ajili ya kuosha mifungo ya wananchi" Ameongeza Mhe. Senyamule

Kadhalika, Mkuu wa Mkoa amewataka wananchi hao kufanya maendeleo kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza kwani mgogoro umekwisha hivyo kutokana na miundombinu itakayojengwa kwenye eneo hilo, itawawezesha kupiga hatua kubwa kwa haraka na kumfanya Mhe. Rais kujivunia kuwapatia eneo hilo.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mji Mhe. Ally Makoa, ameongea na wananchi hao kwa kusema kuwa mapendekezo yao ya kupatiwa eneo la hilo kutoka kwenye mpaka wa Magereza waliyowasilisha kwa Mhe. Rais, ndicho kilichoamuliwa hivyo wananchi hao wataendelea kutumia eneo lao la mashamba huku Magereza nao wakibaki na eneo lilikubaliwa kama ilivyoelekezwa. Hakusita kutoa pongezi zake kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta wataalamu kutoka Wizarani kwa ajili ya kujenga miundombinu kwenye eneo hilo pamoja na kuridhia mapendekezo ya wananchi.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.