Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka (Katikati) akiwa pamoja na wanachama wa chama cha Wafugaji wa Mkoa wa Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka akivishwa shuka la kimasai na Kaniki la kabila la wagogo na Wanachama wa Chama cha Wafugaji wa Mkoa wa Dodoma mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa Chama hicho
Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka na wanachama wa chama cha Wafugaji wa Mkoa wa Dodoma
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Wanachama wa Chama cha Wafugaji wa Mkoa wa Dodoma
Wanachama wa Chama cha Wafugaji Mkoa wa Dodoma wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa chama hicho
................................................................................................
RC MTAKA ATAKA RANCHI YA MIFUGO YA KONGWA IWANUFAISHE WAFUGAJI MKOANI DODOMA
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka ameahidi kukutana na uongozi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kujadili namna ya kuwawezesha Wafugaji wa Mkoa wa Dodoma kunufaika na shamba la Mifugo la Serikali lililopo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma (Kongwa Ranch).
Mhe. Mtaka amesema atazungumza na Wizara ya Mifugo ili wawapatie Wakulima wa Dodoma, vitalu vya ardhi kwenye shamba hilo la Mifugo la Serikali lenye ukubwa wa Hekta 38,000 (sawa na Ekari 95,000) kwa utaratibu wa kukodisha ili Wakulima hao waweze kupata maeneo ya kutosha ya kuendeshea shughuli za ufugaji wa kisasa na uoteshaji malisho ya Mifugo.
Mhe Mtaka amesema kuwa, kipaumbele chake katika sekta ya ufugaji kwenye Mkoa wa Dodoma ni kuendesha ufugaji bora, wakisasa, wenye tija na uwekezaji wa Viwanda vya kuongeza thamani ya Mazao ya Mifugo Kama vile Nyama, Maziwa, Ngozi, Pembe na kwato.
Ameyasema hayo mwanzoni mwa wiki wakati akifungua mkutano wa Wafugaji wa Mkoa wa Dodoma ambao katika Risala yao waliyoisoma kwa Mkuu wa Mkoa Mtaka, wamemlalamikia kukabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maeneo ya kufugia/maeneo ya malisho na kwamba maeneo mengi yaliyopo yana changamoto ya migogoro ya mipaka, ukosefu wa mipango ya matumizi bora ya Ardhi, ukosefu wa huduma muhimu kama maji na majosho ya kuogeshea Mifugo.
Akisoma risala ya Wafugaji, katibu wa Chama cha Wafugaji Mkoa wa Dodoma Bw. Reginaldo Lubeleje amesema kuwa baadhi ya maeneo ya ufugaji na malisho yamekuwa yakivamiwa kwa shughuli za kilimo; Aidha, Wakulima bado wana ukosefu wa Elimu ya Kutosha ya ufugaji bora na kuongeza kuwa kwa hapa Dodoma lipo shamba kubwa la Mifugo la Serikali Wilayani Kongwa (Kongwa Ranch) lakini halina mchango katika kuwasaidia tija Wakulima wa Dodoma na kubadili aina ya ufugaji wao kuwa ufugaji bora na wakisasa.

Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa
Anuani ya Posta: 914 DODOMA
Simu: +255 26 232 4343/232
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz
Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.