• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC SENYAMULE ATOA MAELEKEZO KWA TRC DODOMA SUALA LA FOLENI

Imetumwa : February 17th, 2025

 Na; Happiness E. Chindiye

       Habari - Dodoma RS

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule leo  Februari 17,2025 ametembelea Stesheni ya SGR  ya Samia Suluhu Hassan iliyopo Mkonze  Jijini Dodoma kujionea namna huduma zinavyotolewa, hususani wakati wa kushuka abiria.

Lengo la ziara hiyo ni kutatua changamoto zilizoibuliwa na abiria wanaoshuka eneo hilo na kukumbana na adha ya foleni inayotokana na uwepo wa mageti machache ya kuhakiki stakabadhi za malipo ya ushuru wa vyombo vya moto vinavyotoka katika Stesheni hiyo.

Akizungumza na Uongozi wa TRC Dodoma, baada ya abiria kushuka majira ya saa 07;25 na kujionea hali halisi,Mhe. Senyamule ametoa maelekezo haya.

 “Rais wetu Dk. Samia Suluhu Hassan, ameleta SGR, ni jambo zuri sana lakini sasa tumekuwa tukipokea malalamiko kutoka kwa watumiaji wa Stesheni hii kuhusu kero ya msongamano wa magari unaosababishwa na idadi ndogo ya mashine za kusoma tikeketi za magari wakati wa kutoka.

Naagiza mashine hizi za kuscan magari wakati wa kutoka ziongezeke, lakini pia geti la kutoka litenganishwe kati ya magari na pikipiki ili kupunguza msongamano huu kwani hali hii haipendezi kwenye usafiri huu wa kisasa,”Amesema Mhe. Senyamule

Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa huyo amesema maagizo hayo yafanyiwe kazi ndani ya wiki moja ili kuwaondolea adha watumiaji wa usafiri huo Nchini.


“Nipate taarifa ya utekelezaji wa maagizo haya, wasilianeni na TRC Makao Makuu ili kuona ni kwa namna gani mnaweza kulimaliza suala hili ndani ya wiki moja isifike mwezi mmoja, watu wanapanda treni hii kuokoa muda lakini nyie mnawachelewesha hapa na wengine wana wagonjwa.

Nikiwa hapa hapa nimeshuhudia tumesimama zaidi ya dakika 41 ndiyo gari la mwisho linapita kwenye mashine, sasa kama mimi nipo hapa gari zimetumia muda huo, inakuaje mnapokuwa wenyewe si muda unakwenda zaidi ya huo,”Amesema Mhe. Senyamule

Usafiri wa treni za Umeme  ulizinduliwa rasmi Agosti 1, mwaka 2024 na Rais Samia Suluhu Hassan, na kushuhudiwa na Viongozi wengine wakuu wa Nchi.


&&&


#dodomafahariyawatanzania #keroyakowajibuwangu #birthdayyangumtiwangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • KAMPUNI YA "CAVO'' YA CHINA YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

    May 05, 2025
  • TAWLA - SAUTI YA WANAWAKE NA WATOTO WALIOKOSA ULINZI WA KISHERIA KATIKA JAMII

    May 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.