• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC SENYAMULE AWAPONGEZA MADAKTARI BINGWA NA SHIRIKA LA JAI

Imetumwa : October 12th, 2024

Na. Sizah Kangalawe      
        Habari-DODOMA RS

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amefunga rasmi kambi ya matibabu iliyoendeshwa na Madaktari bingwa na bingwa bobezi wilayani Kondoa mkoani hapa kwa


kuishukuru Taasisi ya  kiislam ‘’JAMIIYAATUL AKHLAAQUL ISLAM (JAI)’’, Benki ya Amana pamoja na madaktari bingwa kwa moyo wao wa kujitolea kuiunga mkono Serikali katika kutoa  huduma za kibingwa na bingwa bobezi kwa watanzania wa hali ya chini na wasiojiweza.


Mhe. Senyamule ametoa pongezi hizo katika hafla fupi ya kuwaaga Madaktari hao iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Morena Oktoba 12/2024 Jijini Dodoma ambapo amewaahidi kuwatengenezea vyeti vya pongezi/ shukrani kwa kutambua mchango walioutoa kwa wananchi wa Wilaya ya Kondoa na Wilaya Jirani.

‘’Sisi Mkoa wa Dodoma tunashukuru kwa huduma yenu, kazi mnayoifanya hatuna cha kuwalipa na kwa kuwa tumefaidika moja kwa moja na huduma hii tutawatengenezea vyeti vya Shukrani kwa kufanya kazi nzuri, tunawakaribisha tena mukipata wasaa wa kututembelea, Karibuni sana’’. Mhe. Senyamule

Akizungumza katika hafla hiyo Kiongozi wa kambi hiyo Dkt. Hussein Msuma,  amesema Wakazi 2,808 wa Wilaya ya Kondoa na Wilaya Jirani, wamepatiwa huduma pamoja na kukamilisha operesheni 73 za kibingwa pasi na kuchangia gharama yoyote.

Kambi hiyo imefanyika kwa juma moja ikiwa na jumla ya mabingwa 26. Ni kambi ya 13 kufanyika kwa uratibu wa Shirika la JAI ambalo huandaa kambi hizo likiwa na dhamira kuu ya kuwasaidia wananchi wasiojiweza kupatiwa huduma za kibingwa, kuwajengea uwezo madaktari na watoa huduma katika vituo husika pamoja na kuhamasisha zoezi la uchangiaji wa damu.


kwa upande wake Mkurugenzi wa Benki ya Amana Bw. Abubakar Athuman Ali, ameahidi kuendelea kudhamini kambi hizo  kwa kushirikiana na Shirika hilo na  watahakikisha watanzania wengi zaidi wenye uhitaji wanafikiwa na kambi hizo katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.



Benki ya Amana inadhamini kambi hizo za matibabu zinazoratibiwa na Shirika la JAI pamoja na Madaktari bingwa toka Hospitali mbalimbali nchini kupitia mfuko wake wa hisani unaojulikana kama Amana Bank Charity Fund.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.