• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC SENYAMULE AAGIZA WATOTO 100 WASIOWASILI SHULENI WATAFUTWE

Imetumwa : February 11th, 2025

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, ametaka hatua za kisheria zichukuliwe kwa Wazazi watakaobainika kuwa hawajawapeleka watoto wao shule mpaka sasa kufuatia taarifa aliyoipokea juu ya watoto 100 ambao bado hawajawasili shuleni tangu kuanza kwa muhula mpya wa masomo.

Hayo yamebainishwa Februari 11, 2025 na Mhe. Rosemary Senyamule alipokua akizungumza na wazazi wakati alipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Mlali Bondeni iliyogharimu shilingi 544,000,000 alipofanya ziara ya kikazi kukagua miradi ya shule katika Wilaya ya Kongwa.

“Lazima tuhakikishe watoto wanakwenda shuleni, hao watoto 100 watafutwe walipo, Mwalimu peleka orodha ya watoto ambao hawajafika shule kwa Mtendaji na ifikapo Jumatatu, nipate taarifa ya wazazi wangapi wameshapeleka watoto shule na wangapi bado, na hatua gani zimechukuliwa.

“Mnaona jengo hili lilivyo zuri? haiwezekani yajengwe vizuri hivi halafu mtoto asiende shule, tutakua tunajikwamisha wenyewe. Wiki hii hapa hapatatulia mpaka watoto hao 100 wafike shule”. Ameongeza Mhe. Senyamule.

Nae, Mbunge wa Jimbo la Kongwa na Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Job Ndugai, alisisitiza suala la elimu kwa watoto wakati wa Mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na wananchi wa Kata ya Sagara.

“Kongwa tumepambana sana katika kukuza elimu na ufaulu wetu umeongezeka. Kwa hiyo tujipange kusomesha watoto, hamuwezi kujua kesho na kesho kutwa watakua kina nani katika Wilaya yetu ya Kongwa na katika nchi hii” Mhe. Ndugai

Katika Mkutano huo, Mhe. Senyamule alisikiliza kero za wananchi wa Kata ya Sagara na kuzipatia majawabu papo hapo kutoka kwa wataalamu alioambatana nao kwenye ziara hiyo huku akitoa maagizo kadhaa kwa baadhi yao kuhakikisha wanatatua kero hizo kwa wakati.

Miradi mingine aliyoitembelea ni ujenzi wa Maabara ya masomo mchanganyiko ya sayansi katika shule ya sekondari Msunjilile inayogharimu shilingi Milioni 60 fedha za ndani za Halmashauri,Mabweni mawili na matundu 10 ya vyoo katika shule ya Sekondari Sejeli kwa gharama ya shilingi 267,000,000


#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • KAMPUNI YA "CAVO'' YA CHINA YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

    May 05, 2025
  • TAWLA - SAUTI YA WANAWAKE NA WATOTO WALIOKOSA ULINZI WA KISHERIA KATIKA JAMII

    May 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.