• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SAMIA INFRASTRUCTURE BOND YACHANGISHA ZAIDI YA BILIONI 1.5 DODOMA

Imetumwa : December 16th, 2024

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS

Kufuatia uzinduzi wa mfuko wa hati fungani unaojulikana kama ‘Samia Infrastructure Bond’ unaolenga kuboresha barabara zilizo chini ya Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) kwa kushirikiana na Benki ya CRDB, harambee ya kuchangia mfuko huo imefanyika leo Desemba 16, 2024, ambapo Mkoa wa Dodoma umechangisha takribani shilingi Bilioni 1.5

Harambee hiyo iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, imefanyika katika ukumbi wa Mabele Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi wa Mkoa wa Dodoma, mikoa ya jirani ya Singida, Morogoro na Iringa pamoja na Taasisi mbalimbali za Umma na Binafsi zilizopo Mkoani hapa.

“Hati fungani hii inalenga kukusanya fedha na kuhakikisha ujenzi wa barabara zetu unakamilika kwa wakati,lakini pia inatoa fursa kwa wawekezaji kupata faida kwa fedha wanazowekeza. Tutumie fursa hii kujenga barabara imara zitakazokamilika kwa wakati na kuinua uchumi” Amesema Mhe. Senyamule.

Kadhalika, Naibu Katibu Mkuu wa OR - TAMISEMI Mhandisi Rogatius Mativila amesema

“Hati fungani hii ni ya kwanza kutolewa Nchini na Mhe. Rais Samia, na inaonesha dhamira yake ya uharaka wa maendeleo ya Watanzania. Bondi hizi zitahusisha Wakandarasi wanaotengeneza barabara za Wilaya tu, sisi ni walengwa na wanufaika wakubwa kuliko wengine”

Aidha, Mwakilishi wa Meneja wa CRDB Kanda ya Kati Bw. Andrew Mheziwa, amesema hati fungani hiyo ni ya miaka mitano ambapo ilizinduliwa rasmi Novemba 09, 2024 na Makamu wa Rais Mhe. Philip Mpango kwa niaba ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na inahusisha kila Mwananchi / Vikundi au Taasisi ambapo kianzio ni shilingi 500,000

Akiongea kwa niaba ya Wakandarasi, Mwenyekiti wa chama cha Wakandarasi Mhandisi Vivian Komu, ameishukuru CRDB na ujio wa mfuko huo kwani wakandarasi wengi watanunua hisa na atakayefaidika zaidi ni mwenye mradi kwani itarahisisha upatikanaji wa fedha na kurahisisha miundombinu ya nchi kwa maendeleo ya Taifa na uzalishaji wa uchumi.

Samia Infrastructure Bond’ ni hati fungani ya kipekee ya miaka mitano yenye riba ya 12% ambapo faida yake inalipwa kwa mwaka mara nne, kila baada ya miezi mitatu na ununuzi wa hati fungani ni kwa kipindi cha mwezi mmoja ambapo zoezi limeanza na litafungwa rasmi Januari 17, 2025 na mfuko huo unatarajiwa kuchangisha kiasi cha shilingi Trilioni 16.


#dodomafahariyawatanzania                                  

#keroyakowajibuwangu

 #mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’ YAIVA

    May 08, 2025
  • DODOMA YADHAMIRIA KUJIKITA KWENYE KILIMO CHA MATUFAHA (APPLES) KUINUA UCHUMI

    May 08, 2025
  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.