• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SENYAMULE AAGIZA WAZEMBE KUCHUKULIWA HATUA KWA MUJIBU WA SHERIA

Imetumwa : July 6th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ametaka hatua kali za kisheria zichukuliwe kwa watumishi wote ambao wamebainika kuhusika na vitendo vya ubadhirifu wa rasilimali au fedha za umma na kusababisha hoja za ukaguzi kwa uzembe.

Akizungumza katika Kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino leo tarehe 07/ 06/2023 Senyamule amekemea vikali tabia ya baadhi ya watumishi kutotimiza majukumu na wajibu wao wa msingi kwa makusudi hali inayopelekea kukithiri kwa hoja za ukaguzi zisizokuwa na majibu.

"Kila mmoja atimize wajibu wake, hoja nyingi hapa zinatokana na uzembe wa baadhi ya watumishi kutotimiza majukumu yao kwa mujibu wa Sheria, wanashindwa kuambatisha nyaraka za msingi zinazohitajika hali inayopelekea kukithiri wa hoja za ukaguzi. Senyamule ameonya.

Amesema ili Halmashauri hiyo kuondokana na hoja nyingi ni lazima Kamati ya Fedha kukutana kila mwezi na kuwa na agenda ya kudumu ya kujadili mwenendo wa  namna ya kujibu hoja za Mkaguzi wa ndani na zile za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na kuchukua hatua stahiki pale inapobainika uzembe wa aina yoyote.

Senyamule pia, ametoa rai kwa madiwani hao kuhakikisha kuwa fedha zinapelekwa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kuzingatia mgawanyo wa asilimia 40 na asilimia 10 kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa mujibu wa Sheria. Pia amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino Dkt. Semistatus Mashimba kuhakikisha mapato ya Serikali yanakusanywa kikamilifu na kudhibiti upotevu.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mapendekezo ya mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kwa Halmashauri ya Chamwino, Bw. Chambi Ngelela Mkaguzi Mkuu wa Nje amesema Halmashauri hiyo ilipata hati inayoridhisha.

"Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino ilikuwa na hoja 61 ambapo hoja 13 zimeweza kufungwa na kusalia na hoja 48 ambazo utekelezaji wake unaendelea." Amesema Bw. Ngelela.

Aidha Senyamule katika hatua nyingine amewataka Viongozi hao wa ngazi ya Wilaya kuendelea kutunza Mazingira na kuanza maandalizi ya kuoteshea vitalu vya miche ya miti kwa ajili ya kupanda wakati wa msimu wa mvua unapokaribia ili kuwe na miche ya kutosha kwa kila Halmashauri kupanda miti milioni moja na laki tano kwa mwaka kwa mujibu wa maelekezo ya Serikali.

"Katika kuendelea kukijanisha Mkoa wetu na kutunza Mazingira tuanze mapema maandalizi ya kuandaa vitalu vya miche na kila wilaya iwe na Miche ya kutosha isiyopungua milioni moja na laki tano. Hapa nisisitize kuwa katika kila wilaya nitakayofanya ziara kuanzia mwezi wa nane nitakagua vitalu hivyo vilevile hakikisheni mnatenga maeneo kwa ajili ya kunufaika na biashara ya hewa Ukaa na kila Wilaya angalau iwe na maeneo matatu kama tulivyokubaliana hapo awali". Amesisitiza Senyamule

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.