• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SENYAMULE AKUTANA NA WADU LA ZAO LA ZABIBU KUWEKA MIKAKATI ILI KUIMALISHA ZAO HILO

Imetumwa : May 16th, 2023


 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule hii leo 16 Mei,2023 amekutana na kufanya mazungumzo na wadau wa zabibu kwa lengo la kujadili fursa na changamoto zinazokabili zao hilo  ili kulipatia ufumbuzi, katika ukumbi wa Jakaya Mrisho Kikwete jijini Dodoma.

Katika kikao hicho kilichohusisha wakulima na wanunuzi wa zao hilo na kuhudhuriwa na Mhe. Anthony Mavunde Naibu Waziri Wizara ya Kilimo, Mhe. Deogratius Ndejembi Naibu Waziri Ofisi ya Rais ,Tawala za Mkoa na Serikali za Mtaa (TAMISEMI), Mhe. Kenneth Ernest Nollo Mbunge wa Jimbo la Bahi, Bw. Ally Gugu Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Wakuu wa Wilaya tatu Chamwino, Bahi,na Dodoma Mjini kimefikia maamuzi ya kuinua zao hilo.

Senyamule amewataka washiriki wa kikao hicho kuhakikisha wanashirikiana vizuri ili kuweza kuleta Maendeleo ya ndani ya Mkoa na taifa kwa ujumla.

"Ushirika ndio matumaini makubwa katika kutupa nguvu ya pamoja na kuweza kukua katika kilimo, nendeni mkasimamie na kutekeleza kwa makini maazimio tuliyokubaliana kwa kuwa tukishirikiana tutafika mbali", Amesisitiza Senyamule

Aidha, Mheshimiwa Senyamule amewataka wakulima wa zao hili kutumia utalaamu wa kisasa ili kuendana na mazingira ya sasa na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu, na kusisitiza matumizi ya mbolea katika kuimarisha upatikanaji wa mazao na kuongeza tija katika uzalishaji. Senyamule pia ameipongeza Kampuni ya Jambo Food Products kwa kazi nzuri wanayofanya ya uchakataji wa zao hilo na ameahidi kuwapa eneo kwa ajili ya kuanza Ujenzi wa Kiwanda Mkoani Dodoma.

Kwa Upande Wake, Mhe. Anthony Mavunde Naibu Waziri Wizara ya Kilimo ametoa wito kwa wakulima wa zao la zabibu na wachakataji kufanya ukulima wenye tija kwa kuzingatia maelekezo ya maafisa ugani kwakuwa zao hili limeongezeka thamani kulingana na jitihada za serikali za kuwatafutia masoko ya uhakika wazalishaji na wakulima wa zao hilo. 

’’Serikali hatuwezi kuweka siasa kwenye Maisha ya watu lazima mikakati yetu ijibu changamoto zinazowakabili wakulima ili mwisho wa siku waweze kwenda mbele kwa kuuza mazao yao ndani na nje ya nchi’’amefafanua Mavunde

Nae, Emmanuel Ngusa Meneja Masoko wa Kampuni ya Jambo Food Product  amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa ushirikiano na dhamira yake juu ya zao la zabibu na amesema lengo la kampuni  mwaka huu  ni kuendeleza  mshikamano kwa wakulima kwa kuanza kununua zabibu kwa muda muafaka Watanunua kwa muda muafaka ambapo kwa msimu huu wanatarajia kununua tani 3000 za zabibu.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.