• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TATU KUBWA ZA MKOA WA DODOMA, SIKU YA KUZALIWA RAIS MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN

Imetumwa : January 27th, 2023

Mkoa wa Dodoma umeadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha matukio makubwa matatu ya kimkakati ambayo yameweka kumbukumbu ya kudumu kwa jamii na matokeo chanya

Matukio hayo ni pamoja na changizo la kugharamia wanafunzi wenye mahitaji maalumu, uzinduzi kwa kituo jumuishi kwa manusura wa ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto kilichopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na zoezi la upandaji miti.

Kiasi cha shilingi Milioni 92.8 zimepatikana katika chakula cha hisani kilichoandaliwa maalumu kusheherekea siku ya kuzaliwa ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya kuchangia gharama za masomo wanafunzi wenye uhitaji takriban 1,128 kutoka mikoa 26 ya Tanzania bara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule katika hafla ya kuchangia Mfuko wa Kichungaji wa Elimu Mtwara (Mtwara Pastoral Education Fund - MPEF) ametoa rai kwa jamii kuhakikisha wanawezesha wanafunzi wahitaji kusoma ili kufikia ndoto zao.

Katika hafla hiyo Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amechangia kiasi cha Shilingi Milioni 50 huku milioni 42.8 zikichangwa na wageni walioalikwa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amezindua kituo cha utoaji huduma jumuishi kwa manusura wa ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto kilichopo hapa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Akizindua kituo hicho Mhe. Senyamule amesema Mkoa wa Dodoma ni kati ya Mikoa yenye changamoto za matukio ya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya Watoto, hivyo kituo hicho cha kwanza katika Mkoa kitasaidia manusura wa ukatili ambao watapata huduma zote kwa haraka kwa wakati muafaka.

Amesema lengo la kuanzishwa kwa kituo hicho ni kurahisisha mfumo wa rufaa kwa manusura katika kupata huduma maalumu zingine kama vile huduma za afya, Ustawi wa Jamii na huduma za msaada wa kisheria.

“Hakikisheni kituo hiki kinafanya kazi masaa 24 ili kurahisha huduma na kutumiza malengo ya uanzishwaji wake” Alisisitiza Mhe. Senyamule.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Dodoma alijumuika na jumuiya ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) katika zoezi la upandaji miti takribani 400 katika eneo la Vikonje ambapo makao makuu ya TBC yanajengwa.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.