• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAAJIRI SEKTA BINAFSI,TOENI MIKATABA KWA WAFANYAKAZI WENU-RC SENYAMULE

Imetumwa : May 1st, 2024

Waajiri sekta binafsi Mkoa wa Dodoma, wametakiwa kufuata Sheria na taratibu za uajiri ikiwa ni pamoja na kulinda haki za wafanyakazi wao kwa kuhakikisha wanatoa Mikataba ya kazi kwa wafanyakazi wao ili waweze kupata stahiki zao muhimu pindi muda wa ajira unapokwisha.

Hayo yamebainishwa leo Mei Mosi, 2024 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule kwenye hotuba yake kwa wafanyakazi wa Taasisi za umma na binafsi waliojitokeza kushiriki Maadhimisho ya Sherehe za wafanyakazi (Mei Mosi) Kimkoa kwenye uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

"Serikali ina thamini mchango wa wafanyakazi ndio maana tunaadhimisha siku hii. Nitoe wito kwa waajiri sekta binafsi kuhakikisha wanatoa mikataba ya ajira kwa wafanyakazi wao na pia kuhakikisha wanapeleka mafao yao kwenye mifuko ya hifadhi za jamii.

"Waajiri ambao watakiuka hili, nitoe shime kwa mifuko hiyo kufuata taratibu za kisheria dhidi ya waajiri wasiowasilisha mafao hayo. Pia , niwasisitize Watumishi wachache wasiotimiza wajibu wao, timizeni wajibu kwa Sheria na taratibu za utumishi " Amesema Mhe. Senyamule.

Kadhalika, Mratibu wa vyama vya wafanyakazi Mkoa wa Dodoma Bw. Sylvester Mshanga akisoma risala ya wafanyakazi mbele ya mgeni rasmi, amemshukuru Mhe. Rais kwa kujali vilio vya wafanyakazi kwani katika kipindi cha miaka mitatu amepandisha madaraja kwa Watumishi, ameondoa tozo ya 6% kwa mikopo ya Elimu ya juu, kulipa Watumishi walioondolewa kazini kutokana na changamoto ya vyeti n.k.

Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani maarufu kama Mei Mosi hufanyika kila mwaka nchini na mwaka huu, Kitaifa yamefanyika kwenye Mkoa wa Arusha huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa ndiye mgeni rasmi. Maadhimisho hayo yameongozwa na kauli mbiu isemayo "Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga dhidi ya hali ngumu ya maisha"



#keroyako,wajibuwangu#dodomafahariyawatanzania

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MMUYA AHIMIZA UDHIBITI VIFO VYA MAMA NA MTOTO

    May 26, 2025
  • UHAKIKI ANUANI ZA MAKAZI KUANZA MEI 28 DODOMA

    May 26, 2025
  • WAWEKEZAJI WA VIWANDA KUTOKA DUBAI WABISHA HODI DODOMA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI KUTOKA TUME YA MADINI WAMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.