• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WANANCHI 16,530 KUJIPATIA MITUNGI YA GESI KWA PUNGUZO LA 50%

Imetumwa : January 8th, 2025

 Na. Sizah Kangalawe

Habari- Dodoma Rs

Miongoni mwa agenda za Dunia ni pamoja na  utunzaji wa Mazingira,na kila mmoja anao wajibu wa kuhakikisha hali endelevu ya kuhakikisha mazingira yanatunzwa ipasavyo, katika kuunga juhudi hizo Wizara ya nishati kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wamezindua mradi wa usambazaji mitungi ya Gesi kwa Bei ya ruzuku Ili kuwafikia Wananchi wengi zaidi hususani katika kona zote za Nchi ikiwemo Mkoa wa Dodoma.

Uzinduzi huo umefanywa  Januari 8/2025 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule katika viwanja vya Ofisi ya Kijiji cha Chamwino Ikulu Wilayani Chamwino.

Akizungumza na Wananchi walioshiriki hafla hiyo RC Senyamule amesema" ni Maono ya Mhe. Rais kugawa mitungi 16,530 Kwa wilaya 6 za Mkoa wa Dodoma kwa bei ya ruzuku, haya ni malengo endelevu ya kidunia ya kuhakikisha nishati safi inapatikana kwa bei nafuu na kwa urahisi, thamani tuliyopewa na Rais ni kubwa sana.

"Nitoe rai kwenu Wananchi, nyie mmepewa mitungi hii kwa bei pungufu ya Sh.20,800, kwahiyo niwaombe mchangamkie fursa hii, lakini pia tumieni gesi hizo kulingana na maelekezo mliyopatiwa hapa na wataalam", amesema Senyamule.

Aidha RC Senyamule amewataka Wananchi kuwa makini na watu wasiowaaminifu na wasio na nia njema ambao watatumia fursa hiyo Kuwatapeli kupitia vitambulisho vyao vya Taifa na kujiingizia fedha kinyume na taratibu.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Janeth Mayanja ametoa Rai kwa  Wananchi kuchangamkia fursa ya ruzuku ya majiko  hayo na kuahidi kuwa Wilaya hiyo watakuwa mabalozi wazuri wa Nishati safi ambapo kuyatimiza hayo wameanzisha kampeni ya "nitunze nikutunze" ambayo inahamasisha kila kaya kupanda miti kuanzia mitano nakuendelea.

Naye kaimu Meneja REA Bw. Emmanuel Yessaya amesema mradi huo unagharimu zaidi ya million  813 na mitungi hiyo ya kampuni ya 'lake gas' inauzwa kwa Bei pungufu ya 50% ambapo mtungi wenye gesi utauzwa kwa Sh. 20,800 pekee na zaidi ya mitungi laki nne itasambazwa Nchi nzima.

Hayo yamejiri ikiwa ni utekelezaji wa adhma ya Rais wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuwa ifikapo 2030 zaidi ya 80% ya watanzania wawe wanatumia nishati safi na kuepukana na matumizi ya nishati chafu.

Awali Wananchi hao wamepatiwa elimu juu ya matumizi sahihi ya Nishati ya Gesi ili kuepukana na madhara ya kulipuka kwa moto kunakotokana na matumizi yasiyo sahihi ya gesi, elimu hiyo imetolewa na Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Dodoma.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WAZAZI WASISITIZWA KUPELEKA WATOTO SHULE KUFUATIA KUIMARIKA KWA MIUNDOMBINU YA ELIMU

    May 08, 2025
  • WATUMISHI HODARI 2025 KUTOKA OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA WAPONGEZWA

    May 09, 2025
  • MRADI WA KUIMARISHA HUDUMA ZA KIFAFA WAZINDULIWA DODOMA

    May 08, 2025
  • UBALOZI WA UINGEREZA NCHINI TANZANIA WAADHIMISHA MAFANIKIO YA MWAKA MMOJA NCHINI

    May 08, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.