• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WANAWAKE KANDA YA KATI WASISITIZWA KUFUATA NYAYO ZA DKT.SAMIA

Imetumwa : March 4th, 2025

Na. Hellen M. Minja,

Habari - DODOMA RS


Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wake Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, inaendelea kufanya jitihada mbalimbali kuhakikisha Wanawake wanashiriki kugombea nafasi za uongozi Serikalini kuanzia ngazi za chini na zile za juu kwani imethibitishwa kuwa wanaweza kupitia nafasi ya juu aliyoipata Mhe. Rais nchini.


Hayo yamebainishwa na Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anna Makinda, alipokua akizungumza na Wanawake waliojitokeza kwenye Kongamano la Wanawake kuelekea siku ya Wanawake Duniani kwa Mikoa ya Kanda ya Kati lililofanyika katika kituo cha Mikutano Jakaya Kikwete Jijini Dodoma Machi 03, 2025.


"Serikali kupitia Rais Samia Suluhu Hassan, imesisitiza ushiriki wa Wanawake katika nafasi za uongozi. Jitihada hizi ni kutokana na Rais wetu kuwa kinara kuhakikisha Wanawake wanashiriki kugombea nafasi za uongozi Serikalini kwa kuendelea kutambua na kuhakikisha changamoto za Wanawake zinasikika" Mhe. Anna Makinda


Kadhalika, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, anayeshughulikia Makundi maalum Wakili Amon Mpanju, amesema Maadhimisho ya mwaka huu yatakwenda sambamba na tathmini ya miaka 30 ya Beijing hivyo, Wanawake wataweka mikakati ya kuhakikisha wanafikia usawa wa maendeleo yao na jamii kwa ujumla.


Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amempongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwani yeye ndiye chachu ya Wanawake kujivunia leo huku akitoa takwimu za viongozi Wanawake katika Mkoa wake.


"Mkoa unaongozwa na viongozi Wanawake ikiwemo Mimi Mkuu wa Mkoa 100%, Wakuu wa Wilaya 71%, Makatibu Tawala Wilaya 86%, Wabunge wa Majimbo 11%, Wakurugenzi wa Halmashauri 25%, Madiwani 14%, Watendaji Kata 38%, Watendaji wa Vijiji 49% na Wenyeviti wa Vijiji na mitaa ni 5% hivyo tunayo kazi ya kuwajengea uwezo Wanawake wenye viti wa Mitaa kujitokeza zaidi". RC Senyamule


Kongamano la Wanawake kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani Machi 08, 2025  yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Arusha, ni maalum kwa kuwa limeendana na mada kama vile, namna taasisi za elimu ya juu zinavyosaidia wanafunzi wa kike kushika nafasi za uongozi, jinsi ya kupambana na rushwa ya ngono kazini, uwezeshaji Wanawake kiuchumi na kupinga ukatili wa kijinsia.


Kongamano hilo la Kanda ya Kati, limehusisha Mikoa ya Singida, Dodoma na Iringa huku likisimamia Kauli mbiu ya "Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji" na kuongozwa na mada kuu ya "Wanawake na Uongozi katika miaka 30 ya Beijing"




#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MMUYA AHIMIZA UDHIBITI VIFO VYA MAMA NA MTOTO

    May 26, 2025
  • UHAKIKI ANUANI ZA MAKAZI KUANZA MEI 28 DODOMA

    May 26, 2025
  • WAWEKEZAJI WA VIWANDA KUTOKA DUBAI WABISHA HODI DODOMA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI KUTOKA TUME YA MADINI WAMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.