• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WANAWAKE TAASISI ZA ELIMU YA JUU TAIFA 2024 WAKUTANA DODOMA

Imetumwa : September 12th, 2024

Umoja wa Kamati ya Wanawake THTU Taifa imefanya mkutano wake wa mwaka 2024 wenye lengo la kuwaleta pamoja wanawake viongozi katika Taasisi za elimu ya juu Tanzania. Mkutano huo wa siku mbili unafanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Mkutano huo uliofunguliwa na Mheni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosermary S. Senyamule, umehusisha mawasilisho ya mada mbalimbali zikiwemo likizo za uzazi na unyonyeshaji pamoja na masuala ya bima ya afya.

Katika hotuba yake, Mkuu wa Mkoa huyo ametaja mambo mbalimbali yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita katika kuimarisha taasisi za elimu ya juu.

“Serikali imeongeza fedha kwa ajili ya ufanyaji tafiti kwa dhamira ya kuwawezesha wasomi kutupatia majawabu, kuna miradi ya HIT ya kuimarisha miundombinu ya chuo na kufanya mazingira bora ya kusomea kwenye vyuo na vyuo vikuu.

“Aidha Serikali imeongeza mikopo ya elimu ya juu ambapo haya yote yatangeza chachu kwa wasomi hawa kuongeza bidii kwenye masomo yao kwani tayari wazazi wamepunguziwa mzigo. Ukiwa mwanamke una wajibu mkubwa wa kuonesha uwezo wako kuliko hata mwanaume” Amesema Mhe. Senyamule.

Katika hotuba yao, wanawake hao wameiomba Serikali kuboresha kikokotoo ili mfanyakazi anapostaafu apate 50% ya mafao yake kwani itatoa motisha kwao kuishi maisha ya staha baada ya kustaafu pia ihakikishe wafanyakazi wote wananufaika na ongezeko la mshahara.

Kadhalika, Mratibu Mkuu wa Kamati hiyo Taifa Bi. Salma Fundi, amesema kuwa mikutano hiyo ya mwaka huwawezesha wanawake kupeana elimu, uwezo na kuwasilisha changamoto wanazokumbana nazo mahali pa kazi kwa mwaka mzima.

Mkutano huo wa mwaka 2024 ulioanza Septemba 12 hadi 13, umeongozwa na kauli mbiu isemayo, “Uwezeshaji wa mwanamke, uboreshaji wa kikokotoo na mfuko wa bima ya afya kwa ajira bora, afya imara na ushiriki wa kidemokrasia 2024”

#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.