• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WATOA HUDUMA ZA MALAZI NA USAFIRISHAJI WAASWA KUTOA HUDUMA BORA KWA WAGENI

Imetumwa : January 13th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari, DODOMA RS

Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya, Januari 13, 2025, alikutana na watoa huduma za malazi na usafirishaji Jijini Dodoma, kuzungumzia namna ya kuimarisha na kuboresha utoaji huduma kwa kuzingatia Mkoa wa Dodoma unakwenda kupokea wageni wengi kipindi hiki cha kuelekea mkutano mkuu maalum wa CCM Taifa utakaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Januari 18 na 19 .

Akifungua kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma jengo la Mkapa Jijini humu, Katibu Tawala huyo amesema Mkoa wa Dodoma ndio wenye fursa nyingi za uwekezaji kwani utaendelea kupokea wageni wengi kadri miradi mikubwa ya maendeleo inavyokwenda kukamilika.

"Dodoma ndio Mkoa pekee wenye fursa mbichi na ndio maana tunahitaji uwekezaji kwenye maeneo ambayo shughuli zote za mikutano zitafanyikia kwa maana ya hoteli, kumbi nzuri, maeneo mazuri ya chakula na sehemu za starehe hivyo tuache uoga, tuwekeze kwani pia miradi mingi ya maendeleo inafanyika hapa ambayo inatengeneza fursa zaidi" Bw. Mmuya.

Aidha, Mwenyekiti wa Wamiliki wa Hoteli Jijini Dodoma Bw. Wellington Maleya, amesema kuwa Wamiliki wa Hoteli na nyumba za kulala wageni, wanapaswa kuajiri wahudumu wenye uzoefu na maadili mazuri kwani kumekua na malalamiko juu ya watoa huduma wasioridhisha kwenye baadhi ya sehemu hizo hali inayosababisha kushuka kwa biashara.

Vilevile, Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva Pikipiki na Bajaji Dodoma (UMAPIDO) Bw. Chacha Marwa, ameiomba Serikali ya Mkoa kuchukua hatua kwa kusimamia matengenezo ya miundombinu ya Barabara za Jiji pindi zinapopata hitilafu, usafi wa mazingira pamoja na ujenzi unaozingatia mipango miji kwani hayo yanasaidia kulifanya Jiji kuwa na thamani.


#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’ YAIVA

    May 08, 2025
  • DODOMA YADHAMIRIA KUJIKITA KWENYE KILIMO CHA MATUFAHA (APPLES) KUINUA UCHUMI

    May 08, 2025
  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.