• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAZAZI WATAKIWA KUWAPELEKA SHULE WATOTO WOTE WENYE SIFA JANUARI 2025

Imetumwa : November 7th, 2024

Na. Hellen M. Minja,

       Habari - DODOMA RS

Wito umetolewa kwa wazazi na walezi kuhakikisha ifikapo mwezi Januari, 2025, mwanzo wa muhula mpya wa masomo, wanawapeleka shule watoto wote wenye sifa za kujiunga na kidato cha kwanza kutokana na ujenzi unaoendelea wa shule mpya ya Sekondari Simbachawene katika Kata ya Luhundwa, Kijiji cha Kidenge.

Hayo yamebainishwa Novemba 06, 2024, na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule alipoitisha mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata hiyo baada ya kukagua ujenzi wa Shule ya Sekondari Simbachawene katika Kijiji hicho ikiwa ni ziara yake ya kikazi aliyoifanya katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.

Mhe. Senyamule amewataka wazazi kuwapeleka watoto wao shule kwa wingi kwani shule inajengwa kijijini kwao, hivyo itapunguza kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo katika Vijiji vya Jirani.

"Maadam tumeletewa shule karibu, watoto wote waliofaulu, wazazi hakikisheni wanakwenda shule. Pasiwepo na Mtoto aliyefaulu ambaye hatakwenda shule. Nataka tija, tuone matunda ya fedha za Serikali zilizotolewa kwenu na Mhe. Rais" Amesema Mhe. Senyamule.

Akisoma taarifa ya mradi wa shule hiyo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Luhundwa Frank O. Kawonga, amesema shule yake ilipokea shilingi 544,225,626 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya Simbachawene kwa lengo la kupunguza msongamano kwenye shule ya Sekondari Luhundwa.

Mradi wa Shule hiyo utajengwa miundombinu 11 ambayo ni vyumba vya madarasa 4, ofisi 1, jengo la Utawala, Maabara ya kemia na baiolojia, Maabara ya fizikia, maktaba, chumba cha TEHAMA, vyoo vya wanafunzi wa kiume matundu 4, vyoo vya wanafunzi wa kike matundu 4, kichomea taka pamoja na tenki la maji la ardhini.

Aidha, Mkuu wa Mkoa alitembelea mradi mwingine wa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Sijila iliyopo katika Kata ya Pwaga,ambao unatekelezwa  kwa gharama ya shilingi 544,225,626 ambapo mradi huo kwa sasa umefikia asilimia 22 na kazi inaendelea,huku ukitarajiwa kukabidhiwa tarehe 25/12/2025 ukiwa na majengo 11.

Mradi mwingine uliotembelewa ni mradi wa usambazaji huduma ya maji katika Vijiji vya Pwaga, Mingowi, Itende na Maswala. Mradi huo unaogharimu shilingi 4,302,281,669.70 una uwezo wa kubeba ujazo wa lita 75,600 huku ukitarajiwa kunufaisha wananchi takriban 13,971, unasimamiwa na Wakala wa Usambazaji Huduma za Maji Vijiji (RUWASA).

Awali kabla ya kutembelea miradi hiyo, Mkuu wa Mkoa alikabidhi gari mpya kwa Meneja wa RUWASA Wilaya ya Mpwapwa, itakayotumika kurahisisha usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya Maji inayotekelezwa ndani ya Halmashauri hiyo kutokana na ubovu wa gari iliyokuwepo.


#kurayakosautiyako

#ujanjanikupigakura

#dodomatupotayarikupigakura

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’ YAIVA

    May 08, 2025
  • DODOMA YADHAMIRIA KUJIKITA KWENYE KILIMO CHA MATUFAHA (APPLES) KUINUA UCHUMI

    May 08, 2025
  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.