• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

YALIYOJIRI KWENYE UFUNGUZI WA KIKAO KAZI CHA WATENDAJI NA WASIMAMIZI WA ELIMU KATIKA MKOA WA DODOMA LEO JANUARI 3, 2020

Imetumwa : January 3rd, 2020

(Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma)

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge leo Januari 3, 2020 amefungua kikao kazi cha Watendaji na Wasimamizi wa elimu katika Mkoa wa Dodoma ambapo ameziagiza Halmashauri zote nane (8) za Mkoa wa Dodoma kusimamia na kuhakikisha wanafunzi wote 33,803 waliofaulu darasa la saba na kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza wanaripoti shuleni na kuanza masomo ifikapo Januari 6, 2020 shule zinapofunguliwa.

Dkt. Mahenge ametoa kauli hiyo kwenye kikao kazi cha Watendaji na Wasimamizi wa elimu kwenye Mkoa wa Dodoma kilichohusisha Sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma idara ya elimu, Mdhibiti ubora wa shule Kanda ya Kati, Maafisa elimu, taaluma Mkoa na Wilaya za Dodoma kwa upande wa msingi na sekondari, Makatibu wa Tume ya Utumishi ya Walimu na Wadhibiti ubora wa elimu wa Wilaya zote Mkoani Dodoma.

Dkt. Mahenge pia aliwataka kupitia kikao hiko, kuhakikisha wanatoka na mikakati ya kuinua hali ya elimu kwenye Mkoa na kuinua kiwango cha ufaulu wa mitihani ya Taifa ya elimu ya msingi na sekondari (Darasa la saba na Kidato cha nne) kwa kuwa bado hali na kiwango cha sasa hakiridhishi.

“Japokuwa Mkoa unapandisha ufaulu kila mwaka, lakini bado hairidhishi, kwa mfano, katika mtihani wa kuhitimu kidato cha nne mwaka 2018 Mkoa ulishika nafasi ya 21 Kitaifa na upande wa elimu ya Msingi ufaulu wa Mkoa kwa mwaka 2019 ulikuwa asilimia 74.69 na hivyo Mkoa kushika nafasi ya 23 ukiulinganisha na mikoa mingine” alibainisha Dkt. Mahenge.

Dkt. Mahenge alitanabaisha kuwa elimu kwenye Mkoa wa Dodoma ndio kipaumbele cha kwanza na kuishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa namna inavyoendelea kuwekeza kwenye elimu kwa kutoa elimu bila malipo kuanzia awali, msingi hadi sekondari kidato cha nne na ujenzi wa miundombinu ya kutolea elimu. Alisema nchi nyingi za Afrika bado ziko nyuma kimaendeleo kwa sababu bado zinakabiliwa na changamoto ya kuwa nyuma kwenye nyanja za elimu, sayansi na teknolojia.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Maduka Kessy amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa atasimamia maelekezo yaliyotolewa na kamati ya ushauri ya Mkoa inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa iliyoagiza kuandaliwa na kufanyika vikao vya wadau wa elimu wa Wilaya zote saba za Mkoa wa Dodoma na Kikao cha Wadau wa Elimu wa Mkoa mzima ili kupata jukwaa la kujadili changamoto za kielimu na kuziwekea mkakati wa kuendelea kuzishughulikia ili Mkoa uchukue hadhi inayostahili kwenye elimu ikiwa ni Makao Makuu ya Nchi.

RC Dkt. Mahenge akifungua kikao kazi cha Watendaji na Wasimamizi wa elimu Mkoa wa Dodoma

Watendaji na Wasimamizi wa elimu kwenye Mkoa wa Dodoma wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Dkt. Mahenge (hayupo pichani) 

Majadiliano yakiendelea kwenye kikao cha Watendaji na Wasimamizi wa elimu Mkoa wa Dodoma

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Maduka Kessy (kushoto) akitoa neno la kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kufungua kikao kazi cha Watendaji na Wasimamizi wa elimu kwenye Mkoa wa Dodoma


Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • DODOMA YADHAMIRIA KUJIKITA KWENYE KILIMO CHA MATUFAHA (APPLES) KUINUA UCHUMI

    May 08, 2025
  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • KAMPUNI YA "CAVO'' YA CHINA YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

    May 05, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.