• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

JAMII YAASWA KUZINGATIA MAKUNDI 6 YA VYAKULA KATIKA MILO YA WATOTO

Imetumwa : June 10th, 2025

Na; Happiness E. Chindiye    

Habari - Dodoma RS

Wataalam wa Lishe kutoka Wizara ya Afya wamewashauri wazazi na Walezi hasa wenye watoto walio na umri wa kuanzia Miezi 6 kuepuka kuchanganya nafaka zaidi ya moja kwa ajili ya kutengeneza unga wa lishe na badala yake wawaandalie mlo unaotokana na mchanganyiko wa makundi 6 ya vyakula.

Ushauri huo umetolewa tarehe 06.06.2025 wakati wa mwendelezo wa kampeni ya kuhamasisha ulaji wa vyakula vilivyoongezwa virutubishi kwa makundi mbalimbali wakiwemo Mama Wajawazito, wenye watoto chini ya miaka 5 na wanafunzi wa shule za sekondari.

Wakizungumza na Wakina Mama waliohudhuria Kliniki katika Hospitali ya Mtakatifu Gemma Jijini Dodoma  wataalam hao wameeleza kuwa bado jamii haina uelewa kuhusu aina ya vyakula na makundi yake.

“Tuna aina sita ya makundi ya vyakula na hayo ndio tunasisitiza wakati wa kuandaa mlo kila kundi liwekwe, ukitamani sana kubadilisha fleva basi ziwe tu mbili zisizidi zaidi ya mbili ” . - Afisa Lishe jiji la Dodoma Bi. Eva Semeni  Juma

Kuhusu ulaji wa vyakula vilivyoongezwa virutubishi, wataalam hao wamesema baadhi ya vyakula hivyo ni mbadala hasa kwa Mama Wajawazito wanaokutana na changamoto pindi wanapotumia vidonge vya Fefo.

“ Kupitia kampeni hii tunawahamasisha kutumia unga wa ngano na mahindi ambao ndani yake kuna kirutubishi cha pholic “ - Afisa Ustawi wa Jamii wizara ya Afya Bw. Denis Komba

Baadhi ya Wakina mama waliopatiwa elimu hiyo wameeleza namna watakavyoitumia kwao na watoto wao.

“Kwa sasa wizara imejitahidi imeleta vyakula vyenye virutubishi unga wa ngano , unga wa mahindi , mafuta na chumvi “-Mnufaika mafunzo ya lishe Bi. Nuru Hamidu

“ Tumefundishwa kuchanganya vitu vingi kwa lishe ya mtoto siyo vizuri kwani inasababisha mtoto kuwa na udumavu , haina haja tena ya kuchanganya vyakula kundi moja kwa lishe ya mtoto” -Mnufaika Mafunzo ya Lishe Bi. Restuta  Juvenalus

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA YAPONGEZWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA 2023/2024

    June 13, 2025
  • KIWANDA CHA NONDO KINACHOTUMIA UMEME JUA KUJENGWA CHAMWINO MKOANI DODOMA

    June 13, 2025
  • RAIS DKT. SAMIA KUFANYA ZIARA JIJINI DODOMA

    June 13, 2025
  • DODOMA YAENDELEA NA MAANDALIZI KUELEKEA SIKU YA KUPINGA DAWA YA KULEVYA DUNIANI

    June 12, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.