• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KAMPENI YA “MTI WANGU , BIRTHDAY YANGU”; MITI 170 YAPANDWA CHUO KIKUU DODOMA

Imetumwa : October 18th, 2024

Na. Hellen M. Minja,

       Habari DODOMA RS


Miti 780 imepandwa kwenye eneo lenye ukubwa wa ekari Saba (7) wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni ya 'Mti wangu birthday yangu' iliyoasisiwa na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar Mmuya na kuzinduliwa Oktoba 18, 2024, ikiwa na lengo la kuifanya Dodoma kuwa ya kijani  kwa kupanda miti katika kumbukizi ya siku ya kuzaliwa.


Kampeni hiyo iliyozinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule, imefanyika kwenye eneo la Jakaya Kikwete Square ndani ya Chuo kikuu cha Dodoma ambapo imewakutanisha wazaliwa wa mwezi Oktoba kutoka Taasisi mbalimbali, wadau wa Mazingira, wasanii na wanafunzi ambapo miti imepandwa ndani ya eneo hilo.


Akizindua Kampeni hiyo, Mhe. Senyamule amehamasisha siku za kuzaliwa ziwe maalum kwa ajili ya kupanda miti pamoja na kusisitiza Halmashauri na mtu mmoja mmoja kuzingatia agizo la upandaji miti hasa kipindi hiki cha kuelekea msimu wa mvua.


"Kutokana na juhudi za utunzaji Mazingira, mpaka sasa miti Milioni 25 imeshapandwa Mkoani humu. Kupitia Mpango huu, tunakwenda kurasimisha upandaji miti siku ya 'birthday' kwa kila mwezi na kwa maeneo maalum. Nisisitize kila Halmashauri na mtu mmoja mmoja kuanza kuandaa maeneo ya upandaji miti kukamilisha agizo la kupanda miti Milioni 1 na nusu kwa mwaka" Amesema Mhe. Senyamule


Hata hivyo, Bw. Mmuya amehimiza wananchi kupanda miti kwa wingi kadri wawezavyo na ikiwezekana kwa idadi ya miaka wanayotimiza katika mwaka husika kwani kufanya hivyo itakua faida kwa vizazi vijavyo kuepukana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.


"Kuna uhusiano mkubwa kati ya wanadamu na Mazingira. Mungu alifanya miti itumie hewa chafu inayotolewa na wanadamu, nao watumie hewa safi inayotolewa na miti. Kampeni hii na nyingine nyingi zitukumbushe wanadamu juu ya uumbaji wa Mungu kwani jambo hili ni la kiibada" Mhe. Shekimweri.


Aidha, Meneja wa benki ya NMB Kanda ya kati ambaye ndiye mdhamini Mkuu wa kampeni hiyo Bi. Janeth Shango, amesema Taasisi yake itaendelea kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwenye masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo kuhamasisha utunzaji wa Mazingira.


#dodomatwendenitukajiandikishe

#ujanjanikupigakura

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC SENYAMULE AZINDUA NYUMBA YA MWALIMU YA 02 KWA 01 KONDOA

    July 01, 2025
  • RAIS DKT. SAMIA ASISITIZA KUIMARISHWA KWA KILIMO ILI KUJIHAKIKISHIA USALAMA WA CHAKULA

    June 28, 2025
  • SERIKALI IMEJIZATITI KULETA MAENDELEO KWA KUIMARISHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA

    June 25, 2025
  • TANZANIA SIYO SALAMA KWA WAUZAJI , WASAFIRISHA, WALIMAJI NA WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA” - MHE. MAJALIWA

    June 26, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.