• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mhe. Mtaka Afurahishwa na Maono ya Waziri wa Madini na Maendeleo ya Migodi wa Zambia

Imetumwa : June 30th, 2022


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Anthony Mtaka, ameonyesha kufurahishwa na maono ya Waziri wa Madini na Maendeleo ya Migodi wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Paul Kabuswe.

Mhe. Paul Kabuswe akiwa ameambatana na ujumbe wake wametembelea ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa mazungumzo mafupi.

Akiwa ofisi kwa Mkuu wa Mkoa, Mhe. Paul Kabuswe amesema yeye pamoja na ujumbe wake wamejifunza mambo mengi yanayofanyika katika kusimamia na kuendeleza sekta ya madini nchini Tanzania. Amemweleza Mkuu wa Mkoa kwamba, katika ziara hiyo wamefanikiwa kutembelea mgodi wa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu wa Nholi uliopo wilaya ya Bahi mkoani Dodoma kwa lengo la kujifunza namna Tanzania ilivyofanikiwa kupiga hatua kwenye sekta ya Madini hususan kwenye usimamizi wa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu.

Aidha, Waziri Kabuswe amemweleza Mhe. Mtaka kuwa,Tanzania wamepiga hatua kubwa hususan kwenye teknolojia ya uchimbaji mdogo wa madini ambapo ameahidi kurudi tena nchini Tanzania kwa lengo la kujifunza zaidi mnyororo mzima wa shughuli za madini.

” Tukiwa viongozi tumepewa dhamana hivyo ni lazima tufanye mapinduzi ya kiuchumi,kama viongozi wetu waliotangualia walivyopambana kufanya mapinduzi na kuhakikisha tunapata uhuru basi sisi viongozi wa sasa ni lazima tupambane kuhakikisha tunaleta ukombozi wa kiuchumi, ni vyema nchi zote za Afrika zikaungana na kufanya kazi kwa ushirikiano”. Amesisitiza Mhe. Kabuswe.

Akimshukuru kwa kumtembelea ofisi kwake,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Mtaka amempongeza Waziri Kabuswe kwa uamuzi wa kuja kujifunza shughuli za biashara nzima za madini nchini Tanzania.

“Nichukue nafasi hii kukupongeza sana Mhe. Kabuswe, kwani ni viongozi wachache sana wenye maono kama yako.Ingekuwa vyema kama nchi zote 54 za Afrika zingekuwa na mawaziri wenye maono kama yako.Wewe ni wa tofauti kabisa na Zambia wamebarikiwa sana kuwa na Waziri wa aina yako”.

Waziri Kabuswe ameongozana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini na Maendeleo ya Migodi- Bw. Sakwiba Musiwa, Bi. Pamela Nakombe- Afisa Mipango Mkuu na Mhe. Elite.L. Mhone - Mhandisi Migodi Mwandamizi. 

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’ YAIVA

    May 08, 2025
  • DODOMA YADHAMIRIA KUJIKITA KWENYE KILIMO CHA MATUFAHA (APPLES) KUINUA UCHUMI

    May 08, 2025
  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.