• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Ujumbe Toka Burundi Wavutiwa na Machinga Complex- Dodoma,Wapongeza Serikali Ya Tanzania

Imetumwa : July 12th, 2022

Ujumbe wa watu watatu Kutoka nchini Burundi, hivi karibuni umetembelea makao makuu ya nchi ili kujifunza na kujionea maendeleo mbalimbali yanayofanyika jijini Dodoma. Ujumbe huo unaongozwa na Katibu Mkuu  kutoka Chama Tawala Nchini Burundi CNDD – FDD,  Mhe.Reverien Ndikuriyo. Mhe.Ndikuriyo,ameambatana na  Balozi wa Burundi nchini Tanzania Mhe. Gervas Abayeho pamoja na Mshauri wa Katibu Mkuu CNDD-FDD Mhe.Said Kibeya.

Ukiwa jijini Dodoma ujumbe huo, umetembelea  maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Machinga Complex. Katika zira hiyo ujumbe huo toka nchini Burundi umeambatana na mwenyeji wao kutoka Tanzania ambao ni Naibu Katibu Mkuu Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Mhe. Christina Mndeme pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka.

Akizungumzia mradi wa Machinga Complex , Mkuu wa Mkoa wa  Dodoma Mhe. Mtaka ametoa pongezi nyingi sana kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ameridhia ujenzi huo na kuchangia  kiasi cha Tsh.2.5 bil, ambazo zitatumika kumalizia ujenzi wa  mradi huo.

 Mhe. Mtaka ameeleza kuwa pamoja na shughuli za kibishara Machinga Complex ina eneo ambalo wakina mama wenye watoto wanaweza kuwaacha watoto wao hapo wakicheza  na wao kuendelea na biashara, ama pamoja na kuwa na sehemu ya kuhifadhia mali kubwakubwa/stoo Kubwa,wajasiliamali hao waweza kuhifadhi  wenyewe mali zao  ndogondog kwani kwenye kila kibanda kina sehemu ya  kuhifadhia mizigo midogo midogo.

Aidha Mhe. Mtaka mameeleza kuwa ili kulifanya eneo hilo  kuwa rafiki, kutakuwa na vibao kwenye kila jengo vya kuelekeza bidhaa gani inapatikana wapi. Pia kutakuwa na maeneo ya nyama choma, eneo la kutosha la kuengesha magari,maeneo ya huduma za kibenki, kituo cha polisi, mahabusu ndogo,NHIF na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii. Akijibu upatikanaji wa nafasi kwenye vibanda hivyo Mhe. Mtaka alieleza kuwa kigezo cha kupata shehemu hiyo ni kwa mjasiliamali kuwa na kitambulisho cha ujasiliamali ambacho hulipiwa Tsh.20,000/- kwa mwaka aidha pamoja na kitambulisho hicho kuna taratibu zingine ambazo zinatolewa na Jiji la Dodoma.

Sanjali na hayo Naibu Katibu Mkuu CCM Tanzania Bara Mhe. Christina Mndeme amempongeza Mhe. Ndikuriyo, kwa kuamua kutembelea Tanzania, kwani kwa ziara hiyo ameweza kuona njinsi Chama Tawala CCM), kinavyowajali na kuwasaidia Wajasilamali na wafanya biashara ndogondogo

Serikali imetengeneza eneo hili, ili kumlinda mfanyabiashara ndogondogo, sehemu ya watoto kucheza, saloon za kina mama na kina baba, yote haya kusudi kuwawezesha wananchi kiuchumi.Mhe. Rais ametoa fedha kwa Mikoa yote ili kuhakikisha kwamba hawa wafanya biashara wanawekwa  sehemu nzuri.Kama alivyosema Mhe.Mtaka, kusudi la kuhakikisha huduma za kibenki zinapatikana katika eneo hili ni kuwaunganisha wafanya biashara hawa  na mabenki, ili kumsaidia mfanya biashara mdogo baadae awe mkubwa.

Aidha Katibu Mkuu kutoka chama Tawala Nchini Burundi CNDD-FDD Mhe.Reverien Ndikuriyo , ameipongeza sana Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa kuwajali wafanya biashara wake wadogo wadogo na kuwapatia vitambulisho ambavyo kila mmoja wao hulipia  Tsh.20,000/- kwa mwaka.

“Ili uwe mkubwa lazima uanze kuwa mdogo.  Kwa kuwa hii Machinga Complex itatoa fursa ya pekee kwa wafanya biashara wadogo.Bila shaka wafanya biashara wakubwa watafanya biashara na Wafanya biashara, wadogo ili biashara ziweze kutoka  kwa  haraka, kwani idadi kubwa ya watu itakuwa ikija hapa kuliko maduka ya mitaani’’.Amesema Ndikuriyo. Aidha Katibu Mkuu CNDD-FDD amempongeza sana Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa ubunifu na uchapa kazi na kuahidi kutembelea tena Tanzania na hasa Dodoma. MWISHO.

 

 

 

 

 

 

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’ YAIVA

    May 08, 2025
  • DODOMA YADHAMIRIA KUJIKITA KWENYE KILIMO CHA MATUFAHA (APPLES) KUINUA UCHUMI

    May 08, 2025
  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.