• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

ALAT Watembelea Jengo la Machinga

Imetumwa : June 23rd, 2022


Uongozi wa Kamati tendaji za Serikali za Mitaa Tanzania ( ALAT), hivi karibuni umetembelea Ujenzi unaoendelea wa jengo la Machinga  Complex, lililiopo eneo la Bahi Road Jijini Dodoma. Viongozi hao wapo Jijini Dodoma kwa  ajili ya kuhudhuria, vikao vya kiutendaji.Aidha pamoja na vikao hivyo viongozi hao, waliamua  kutembelea jengo la Machinga Complex ili kuliona na kujifunza.

Wakiwa wameambatana na mwenyeji wao, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka, Mhe Mtaka aliwakaribisha kwenye mradi huo na kutoa shukrani na pongezi nyingi  sana kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye aliridhia ujenzi huo na kuchangia  kiasi ctah Tsh.2.5 bil, ambazo zitatumika kumalizia ujenzi wa   mradi huo. Mhe. Mtaka alisisitiza kuwa mradi huu unatakiwa kujenga ujasiri kwa Halmashauri kubuni miradi mingi zaidi kwani watu wa kuiunga mkono wapo.

Akielezea maendeleo ya mradi huo, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Bw. Joseph Mafuru, alisema kwa sasa Ujenzi upo kwenye awamu ya pili ya kukamilika na unatarajiwa kufanya kazi kwa saa 24 na mpaka kufikia Juni 30 mradi utakua umekamilika,ili ifikapo Julai Mosi, mradi uwe umezinduliwa rasmi kwa wafanyabiasha kuanza kuutumia.

Akizungumzia mradi huo, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri amesema kuwa, mradi huo utasaidia Halmashauri ya Dodoma kuongeza mapato, kwani kwa  kipindi cha Mwaka  mmoja, mradi unatarajiwa kuingiza kiasi cha Milioni 100  ambazo zitakazotokana na ushuru wa huduma mbalimbali zitakazokua zikitolewa mahali hapo. Mhe. Shekimweli  ametaka mradi huu kutumika kama Mfano wa kuliweka Jiji katika mwonekano wa kuvutia na utumike kama sehemu ya utalii wa ndani ya Mkoa.

 Mwenyekiti wa ALAT Bw. Murshid Ngeze, alimshukuru Rais Samia  Suluhu Hassan kwa mchango wake kwa mradi huo na kuahidi kuwa watakuja kujifunza kupitia mradi huo. Aidha Bw. Ngeze ameitaka Halmashauri kuhakikisha  kuwa inasimamia vizuri mapato yatakayopatikana kutokana na mradi, kusimamia vizuri hali ya usalama kwenye eneo hilo kwa kuwa Biashara itafanyika kwa saa 24 pia ameshauri kuanzishwa mpango wa kutoa Mafunzo kwa wajasiriamali wanaotarajiwa kufanya biashara katika jengo hilo. MWISHO.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • KAMPUNI YA "CAVO'' YA CHINA YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

    May 05, 2025
  • TAWLA - SAUTI YA WANAWAKE NA WATOTO WALIOKOSA ULINZI WA KISHERIA KATIKA JAMII

    May 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.